Kwa Egypt, hii itakuwa mara ya 4 mfululizo wakijaribu kubeba Ubingwa baada ya kuutwaa Miaka ya 2006, 2008 na 2010 na kutofuzu Fainali za Miaka ya 2012, 2013 na 2015.
Fainali hii ni marudio ya Fainali ya Mwaka 2008 ambayo Egypt na Cameroon zilipambana.
Timu hizo zina Wachezaji kadhaa Maprofeshenali huko Ulaya na baadhi yao wapo huko Uingereza.
Cameroon wanae Kiungo wa Hearts ya Scotland, Arnaud Djoum, na Clinton N'Jie, ambae sasa yupo Marseille akitokea kwa Mkopo huko Tottenham.
Egypt wanao Wachezaji Watatu wanaocheza EPL, Ligi Kuu England, ambao ni Beki Ahmed Elmohamady (Hull City na Viungo Mohamed Elneny (Arsenal) na Ramadan Sobhi (Stoke City), pamoja na Winga wa zamani wa Chelsea Mohamed Salah ambae sasa yupo Italy Klabuni AS Roma.
Egypt wametinga Fainali hii baada ya kuibwaga Burkina Faso 4-3 kwa Mikwaju ya Penati kufuatia Sare ya 1-1 huku Shujaa wao akiwa Kipa mwenye Umri wa Miaka 44 Essam El Hadary.
Cameroon, wakiwa na Timu iliyobadilika baada ya Nyota wao kadhaa kugomea kujiunga nao, wametinga Fainali kwa kuifunga Ghana, iliyopewa nafasi kubwa, 2-0.
AFCON 2017
RATIBA
Robo Fainali
Jumamosi Januari 28
Burkina Faso 2 Tunisia 0 [RF 1]
Senegal 0 Cameroon 0 [Penati 4-5] [RF 2]
Jumapili Januari 29
Congo DR 1 Ghana 2 [RF 3]
Egypt 1 Morocco 0 [RF 4]
Nusu Fainali
Jumatano Februari 1
Burkina Faso 1 Egypt 1
Alhamisi Februari 2
Cameroon 2 Ghana 0
Mshindi wa 3
Jumamosi Februari 4
Burkina Faso 1 Ghana 0
Fainali
Jumapili Februari 5
2200 Egypt v Cameroon
No comments:
Post a Comment