Mourinho akaeleza kuwa yeye alitaka Wachezaji na Mashabiki wao kufurahia ushindi licha ya ukweli kuwa aliweka Historia ya kuwa Meneja wa kwanza wa Man United kutwaa Kombe kubwa katika Msimu wake wa kwanza tu Klabuni hapo.
Pia, Mourinho aliifikia Rekodi ya Sir Alex Ferguson wa Man United na Brian Clough wa Nottingham Forest kuweza kubeba Kombe la Ligi mara 4 huku mara 3 akilitwaa akiwa na Chelsea.
Hivi sasa Man United bado wamo FA CUP na wako Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI.
Licha ya kuwa Nafasi ya 6 ya EPL, LIGI KUU England, Mourinho amekiri Ubingwa kwao Msimu huu kipo nje ya uwezo wao.
No comments:
Post a Comment