Mechi ya kwanza hii Leo ilikuwa huko Old Trafford na Man United kutangulia kufunga kwa Penati ya Kepteni Wayne Rooney katika Kipindi cha Kwanza.
Swansea walisawazisha Kipindi cha Pili kwa Frikiki ya Gylfi Sigurdsson.
Huko Goodison Park, Bao za Kipindi cha Pili za Pedro, Garry Cahill na Willian ziliwapa Chelsea ushindi mnono ambao polepole unawapeleka kutwaa Ubingwa.
Nako huko Riverside, ilikuwa ni vuta nikuvute wakatiu Middlesbrough iliongoza mara mbili na mara mbili Man City kusawazisha.
Boro walitangulia kufunga kwa Bao la Alvaro Negredo na City kurudisha kwa Penati ya Sergio Aguero na kisha Boro tena kupiga la Pili kupitia Callum Chambers na City kusawazisha tena kwa Bao la Gabriel Jesus zikiwa zimebaki Dakika 5.
No comments:
Post a Comment