BAO 2 ndani ya Dakika 3 Leo zimewapa ushindi wa 2-0 Tottenham Hotspurs kwa kuwabwaga Mahasimu wao Arsenal kwenye Mechi yaEPL, Ligi Kuu England, iliyochezwa huko White Hart Lane ikiwa ni Dabi ya Jiji London Kaskazini.Hadi Haftaimu Gemi hii ilikuwa 0-0 lakini Dakika ya 55 kizaazaa Golini mwa Arsenal kulifanya Mpira umfikie Dele Alli alieukwamisha Mpira wavuni.
Chini ya Dakika 3 baadae, Gabriel alimwangusha Harry Kane ndani ya Boksi na Refa Michael Oliver kutoa Penati iliyofungwa na Harry Kane.
Ushindi huu umewachimbia Spurs Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Chelsea huku Gemu zikibaki.
Arsenal wanabaka Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 5 nyuma ya Timu ya 5 Man United.
VIKOSI:
TOTTENHAM: Lloris; Trippier [Walker 88'], Alderweireld, Vertonghen, Davies; Dier, Wanyama; Son [Dembélé 79'], Eriksen; Dele [Sissoko 91'], Kane
Akiba: Vorm, Walker, Wimmer, Dembele, Sissoko, Nkoudou, Janssen.
ARSENAL: Cech; Gabriel [Bellerín 75'], Koscielny, Monreal; Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Xhaka [Welbeck 65'], Gibbs; Ozil, Sanchez; Giroud [Walcott 81']
Akiba: Ospina, Bellerin, Coquelin, Holding, Iwobi, Walcott, Welbeck.
REFA: Michael Oliver
No comments:
Post a Comment