Tottenham itahakikisha Mastaa wao wote wanabakia Klabuni hapo na kuwauza tu wale ambao hawawahitaji kwa mujibu wa Meneja wao Mauricio Pochettino.
Spurs, ambao wako Nafasi ya Pili kwenye EPL, Ligi Kuu England, wanasakamwa na Klabu nyingine zinazowawinda Mastaa wao wakubwa wanaofanya vizuri Msimu huu.
Pochettino amesisitiza: "Wachezaji tunaotaka wabaki watabaki!"
Miongoni mwa wanaosakwa na Klabu pinzani huko England ni Mabeki Kyle Walker na Danny Rose, Viungo Christian Eriksen na Dele Alli na Fowadi Harry Kane.
No comments:
Post a Comment