BUKOBA SPORTS

Wednesday, May 3, 2017

ARSENE WENGER ASISITIZA KUTAKIWA ANG’OKE ARSENAL

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesisitiza kutakiwa aondoke haweki Moyoni na hata yeye binafsi hujichukia wakifungwa.
Wenger, mwenye Miaka 67, hajabainisha kama atasaini Mkataba Mpya mwishoni mwa Msimu huu baada ule wa sasa kumalizika akiwa ameitumikia Arsenal Miaka 20 lakini kipindi hiki anasakamwa mno na Mashabiki ang’oke baada ya Klabu hiyo kushuka nje ya 4 Bora ya EPL, Ligi Kuu England na kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Tangu Wenger atue Arsenal Mwaka 1996 Timu hiyo imekuwa ikimaliza EPL ikiwa kwenye 4 Bora lakini Msimu huu sasa wapo Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 6 nyuma ya Timu ya Nne Man City huku wakiwa wamebakisha Gemu 5.


Huku akisubiri Jumapili kumkaribisha Jose Mourinho na Man United yake hapo Jumapili huko Emirates kwenye Mechi ya EPL, Wenger amesisitiza kupondwa kwake hakuweki Moyoni.

Wenger amenena: “Mie niko kama Watu wote wengine, na napenda nipendwe lakini hilo naliacha. Kwa kweli najichukia mwenyewe kama Meneja kupita yeyote kama sishindi Gemu. Sipendi kufungwa!”
Arsenal hawajatwaa Ubingwa wa England tangu 2004 lakini wametwaa FA CUP mara 2 katika Misimu Mitatu iliyopita.
Lakini Wenger amenyoosha kidole kwa Wapinzani kuonyesha ni ngumu kutwaa Ubingwa.

Ameeleza: “Watu wanataka ushindi. Kama hutwai Ubingwa, FA CUP, CHAMPIONS LIGI, ni maafa. Lakini sie tumebeba FA CUP mara 2 katika Miaka Mitatu na kumaliza Ligi Nafasi za 2, 3 na 4. Safari hii tupo tena Fainali ya FA CUP. Kwa ujumla hatufurahii kwani tunataka tushinde kila kitu!”

Ameongeza: “Lazima ukubali kwamba hata Real Madrid hawajatwaa Ubingwa kwa Miaka Mitano sasa. Ni Klabu kubwa ni ngumu. Liverpool hawajakuwa Bingwa Miaka 20!”

No comments:

Post a Comment