Timu ya Tigo Fc ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi baina yao na timu ya Triple A Klabu Fc kuanza
Timu ya Triple A klabu imelazimika kutoka sara ya bao moja kwa moja na timu ya Tigo FC katika bonanza la michezo lijulikanalo kwa jina la Afya Kwanza lililofanyika katika viwanja vya Gymkana jijini hapa
Bonanza hilo ambalo ni mara ya kwanza kufanyika limeandaliwa na mkurugenzi wa Bendi ya Rickernest music band ,bendi ambayo makao makuu yake ni jijini hapa na imeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba pamoja na mpira wa miguu
Akiongelea bonaza hilo muandaaji wa mashindano hayo Denis Mtedeki alisema kuwa nia rasmi ya kuandaa bonanza hili ni kuwakutanisha watu mbalimbali na kufurahi pamoja pamoja na kushiriki michezo ,ikiwa kama ni sehemu ya kufanya mazoezi
Alisema kuwa bonanza hili limeshirikisha jumla ya timu za mipira wa miguu mbili pamoja na timu zingine mbili ambazo zilifanya kazi ya kuvuta kamba,alizitaja timu hizo kuwa ni timu kutoka kampuni ya simu ya Tigo (Tigo Fc), Olemringaringa FC, Red Apple,Mijada Fc pamoja na Triple a klabu FC.
Denis aliongeza kuwa mbali na kushiriki bonanza hili pia wachezaji na washiriki waliouthuria walipata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali ikiwemo kupima presha na kisukari bure.
Aidha aliongeza kuwa bonanza hili alitaishia hapa bali litakuwa likifanyika kila mwisho wa mwezi lengo ikiwa ni kufanya mazoezi ,kuwakutanisha wadau mbambali mbali na kufurahi pamoja
No comments:
Post a Comment