Akizungumza wandishi wa habari leo, Abdulfareed Hussein alisema kuwa mpambano huo mshindi ataamuliwa na mashabiki baada kimya cha miaka miwili mara ya mwisho kupambana.
“Mshindi ataamuliwa na mashabiki ambao watakuwepo ukumbini siku hiyo na kukabidhiwa zawadi ambayo itatangazwa hapo ukumbini siku hiyo,” alisema Hussein.
Pia Hussein alisema wanaamini lengo la kuandaa pambano hilo dhidi ya bendi hizo kongwe za muziki wa dansi ambazo ni hasimu ni kutoa burudani na kukuza muziki wa dansi.
Akizungumza juu ya pambano hilo Meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti alisema watanzania wajiandae kupata burudani kuanzia enzi za NUTA, JUWATA na OTTU ili wale vijana wa zamani wakumbuke enzi zao.
“Sisi kambi yetu itakuwa Pemba Wete na tukirudi hapa wale vijana wa zamani na wa sasa wajiandae kupata burudani ya ukweli katika ukumbi wa Traventine,” alisema Kibiriti
Naye kiongozi wa Sikinde Abdallah Hema alijigamba kuhakikisha wanatoa buradani isiyo na kifani
No comments:
Post a Comment