Mechi hii inakutanisha Difensi imara dhidi ya Washambuliaji hatari huku Monaco wakisifika kwa kupiga Bao nyingi wakati Juve wakifungwa Goli chache.
Monaco ni Timu yenye Vijana wengi wakati Juve ina Wakongwe na Wazoefu wengi.
Tineja huyo, ambae amefunga Bao 18 katika Mechi 18 zilizopita, hupata sapoti kubwa toka kwa Almamy Toure, Bejamin Mendy, Bernardo Silva, na Nabil Dirar huku Radamel Falcao akiibuka upya Msimu huu na kupiga Bao 28.
Hii ni mara ya kwanza kwa Monaco kutinga Nusu Fainali tangu 2004 lakini mara 2 wamepigwa na Juventus kwenye Mashindano haya ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment