BUKOBA SPORTS

Monday, May 8, 2017

MOURINHO ASEMA 4 BORA NI NGUMU, AKUBALI KICHAPO CHA BAO 2-0 KUTOKA KWA GUNNERS KWA MARA YA KWANZA.

BOSI wa Manchester United Jose Mourinho amekiri kuwa Timu yake kumaliza 4 Bora kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, ni kuwa kitu hakiwezekani baada ya Jana kufungwa 2-0 na Arsenal huku pia akimkejeli Arsene Wenger.Kipugo hicho cha Jana ni cha kwanza kwa Timu inayoongozwa na Wenger kuifunga Timu ya Mourinho katika Mechi 16 zilizodumu Miaka 13.Mourinho ameeleza: "Mashabiki wa Arsenal wamefurahi na mimi nimefurahi kwa ajili yao. Hii ni mara ya kwanza naondoka na wako na furaha. Nlikuwa nkiondoka Highbury wanalia! Nkiondoka Emirates, wanalia!"Aliongeza: "Wanalia wakitembea Mitaani vichwa chini. Ni Klabu kubwa. Unafkiri naskia raha Klabu kubwa kama Arsenal kutoshinda Vikombe? Sisikii raha. Arsene Wenger ni Meneja mkubwa. Kuwa na rekodi ya kutofungwa Mechi nyingi si kawaida!"Kabla ya Mechi hiyo na Arsenal, Mourinho alishakiri nafasi ya Man United kumaliza 4 Bora kwenye EPL ni finyu hivyo njia pekee ni kutilia mkazo kutwaa UEFA EUROPA LIGI ambayo Alhamisi iliyopita waliifunga Celta Vigo 1-0 huko Spain katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali.Alhamisi hii inayokuja Man United itarudiana na Celta Vigo huko Old Trafford.Katika kuonyesha Mechi hii na Arsenal ni kero kwao kwa vile imejichimbia katikati ya Mechi na Celta Vigo, Jana Mourinho alibadili Wachezaji 8 toka Kikosi chake kilichocheza na Vigo na pia kumuanzisha Kinda Tuanzebe na pia Kipindi cha Pili kumuingiza Kinda mwingine, McTominay, Wachezaji ambao hawajawahi kukichezea Kikosi cha Kwanza cha Man United.Licha ya kushusha Kikosi hicho, Mourinho amekiri hawakustahili kufungwa na Arsenal kwani waliidhibiti Mechi hiyo.Kuhusu kumaliza 4 Bora Mourinho ameeleza: "Haiwezekani. Sidhani hao wanaocheza Mechi 1 kwa Wiki watafungwa. Kwa sababu Alhamisi tutacheza kufa na kupona kwenye EUROPA hatuwezi Jumapili kwenda Tottenham tukiwa imara kila kitu. Hivyo 4 Bora hatuna nafasi. Tuikimbize nafasi ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwa kujaribu kutwaa EUROPA LIGI!"Kwa Arsenal, ushindi wao umewaongezea matumaini kwani wana Mechi mkononi.
Hadi sasa Chelsea inaongoza Ligi ikiwa na Pointi 81 kwa Mechi 34 wakifuata Tottenham wenye Pointi 77 kwa Mechi 35, Liverpool ni wa 3 na wana Pointi 70 kwa Mechi 36, kisha Man City waliocheza Mechi 35 na wana Pointi 65. Man United wamecheza Mechi 35 na wana Pointi 65 wakishika Nafasi ya 5 wakifuata Arsenal waliocheza Mechi 34 na wana Pointi 63.

No comments:

Post a Comment