KIPA Mkongwe wa Vigogo wa Italy Juventus, Gianluigi Buffon, anaota kutwaa Kombe la UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, ambalo hajawahi kulibeba.
Baada ya kupoteza Fainali 2 za UCL, Jumanne Usiku Buffon ataiongoza Juve wakiwa kwao Mjini Turin kucheza Mechi ya Pili ya Nusu Fainali ya UCL dhidi ya AS Monaco ambayo waliichapa 2-0 Wiki iliyopita huko Monaco.
Mshindi wa Mechi hiyo atakumbana na Mshindi wa Mechi nyingine ya Nusu Fainali kati ya Atletico Madrid na Real Madrid ambao walishinda 3-0 katika Mechi ya Kwanza kwa Bao zote 3 kupigwa na Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo.
Msimu huu, Buffon ameisaidia mno Juve kusonga hadi Nusu
Fainali ya Mashindano haya wakiwa hawajafungwa Bao hata Moja kwa Mechi 6 sasa.
Kipa huyo ashawahi kutinga Fainali za UCL mara 2 akiwa na Juve na Mwaka 2003 kutolewa na AC Milan na Miaka Miwili iliyopita kubwagwa na FC Barcelona.
Inaelekea hii ndio nafasi ya mwisho kwa Buffon mwenye Miaka 39 kuwania Ubingwa huu wa Klabu Barani Ulaya na mwenyewe amekiri hilo mbali ya kusema bado anafurahia kushindani na Chipukizi kama Straika wa Monaco Kylian Mbappe mwenye Miaka 18.
Buffon ameeleza: “Mbappe amezaliwa Desemba 1998 wakati mie tayari nshacheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 1998 huko France!”
Akicheza Mechi ya Jumanne na AS Monaco, Buffon atafikisha Mechi 150 za UCL.
UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MTOANO:
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

No comments:
Post a Comment