LACAZETTE APIGA BAO MECHI YAKE YA KWANZA HUKO SYDNEY, ARSENAL 2-0 MBELE YA MASHABIKI 80,000
ARSENAL imeanza Ziara yake ya Matayarisho kwa ajili ya Msimu Mpya wa 2017/18 kwa kushinda Mechi yao ya kwanza huko Sydney, Australia walipoichapa Sydney FC 2-0 mapema hii Leo Mchana mbele ya Mashabiki 80,432 ndani ya ANZ Stadium.
Kwa Mashabiki wa Arsenal, furaha kubwa ni kumuona Mchezaji wao Mpya, Alexander Lacazette, akitokea Benchi na kuonyesha cheche zake kwa kupiga Bao la Pili Dakika ya 83.
Bao la Kwanza la Arsenal lilifungwa Dakika ya 4 tu na Beki Per Mertesacker kufuatia kizaazaa cha Kona.
Mechi ya Pili ya Arsenal ni huko huko Australia ndani ya ANZ Stadium Jijini Sydney dhidi ya Western Sydney Wanderers na kisha kupaa kwenda China kuzivaa Bayern Munich na Chelsea.

Arsenal - Mechi kuelekea Msimu Mpya:
13 Julai v Sydney FC, ANZ Stadium, Sydney
15 Julai v Western Sydney Wanderers, ANZ Stadium, Sydney
19 Julai v Bayern Munich (Shanghai Stadium) International Champions Cup
22 Julai v Chelsea (Bird’s Nest Stadium, Beijing)
29 Julai v Benfica, Emirates Stadium (Emirates Cup)
30 Julai v Sevilla, Emirates Stadium (Emirates Cup)
6 Agosti v Chelsea, Wembley Stadium (Community Shield)
No comments:
Post a Comment