Kwenye Mechi hiyo, Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika 2 tu tangu Mechi ianze Mfungaji akiwa Marcus Rashford baada ya mchango wa Jesse Lingard.
Rasford aliongeza Bao la Pili katika Dakika ya 20 na Dakika ya 26 Bao zilikuwa 3-0 Mfungaji akiwa Marouane Fellaini.
Man United waliongeza Bao zao 2 kupitia Henrikh Mkhitaryan na Anthony Martial.
LA Galaxy walifunga Bao zao 2 katika Dakika 11 za mwisho kupitia Giovani dos Santos na Dave Romney.
MAGOLI:
LA GALAXY - Dos Santos 79, Romney 88;
MAN UNITED - Rashford 2, 20, Fellaini 26, Mkhitaryan 67, Martial 72
MAN UNITED - VIKOSI:
Kipindi cha Kwanza: De Gea, Valencia, Jones, Smalling, Blind, Carrick, Herrera, Fellaini, Lingard, Mata, Rashford.
Kipindi cha Pili: J. Pereira, Tuanzebe, Lindelof, Bailly, Darmian, Fosu-Mensah (Mitchell 85), Pogba, A. Pereira, Mkhitaryan, Martial, Lukaku.
Manchester United – Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:
15 Julai v LA Galaxy, Stubhub Centre, Los Angeles [5-2]
17 Julai v Real Salt Lake, Rio Tinto Stadium, Sandy, Utah
20 Julai v Manchester City, NRG Stadium, Houston, Texas (International Champions Cup)
23 Julai v Real Madrid, Levi’s Stadium, Santa Clara, California (International Champions Cup)
26 Julai v Barcelona, FedExField, Washington DC (International Champions Cup)
30 Julai v Valerenga, Ullevaal Stadium, Oslo
2 Agosti v Sampdoria, Aviva Stadium, Dublin
8 Agosti v Real Madrid, National Arena Filip II, FYR Macedonia (UEFA Super Cup)
No comments:
Post a Comment