BUKOBA SPORTS

Sunday, October 29, 2017

NELLY KAZIKAZI ATWAA TAJI LA MISS HIGHER LEARNING 2017


Miss Higher Learning 2017, Nelly Kazikazi, akipunga mkono kwa furaha akiwa na washindi wenzake baada ya kutangazwa rasmi na kuvishwa Taji katika shindano la Miss Vyuo Vikuu lililofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye Ukumbi wa King Solomon Namanga Dar es Salaam. Kulia ni mshindi wa pili, Queen Elizabeth Makune (kushoto) ni mshindi wa tatu, Melody Thomas. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)

Shindano hilo pia lilipambwa na burudani kutoka kwa wasanii tofauti kama JK Comedian Jukwaani, Msaga sumu na Barnaba Boy.

Sehemu ya wageni waliofika kushuhudia shindano hilo wakiwa katika meza za VIP

Shoo ilianza kama hivi kwa kufungua na shoo ya pamoja

JIJI LA TANGA LAZIZIMA KWA FIESTA 2017


Msanii Aslay akitumbuiza mashabiki waliofurika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jumamosi.

Msanii mkongwe wa Taarabu Khadija Kopa na msanii wa bongo fleva, Ben Pol kwa pamoja wakiwa kwenye jukwaa la tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga usiku wa kuamkia jumamosi.

RosaRee akiwa katika jukwaa la Tigo Fiesta
Msanii Zaidi yao akiimba na mashabbiki zake katika Tamasha la Tigo Fiesta Mkoani Tanga.

Msanii wa bongo fleva, Nandy akiwa kwenye jukwaa la tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga usiku wa kuamkia jumamosi.

SIMBA NA YANGA HAKUNA MBABE, ZATOKA 1-1





TAMBO zote za watani wa jadi Yanga na Simba zimeisha kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo.
Timu hizo ziliingia uwanjani zikitoka kushinda mabao 4-0 katika mechi zao za mwisho, Yanga dhidi ya Stand United Shinyanga na Simba dhidi ya Njombe Mji, Uhuru, matokeo ambayo yalitoa hamu kushuhudia mechi yao ya jana kila mmoja akitaka kufahamu nani ni zaidi ya mwingine.
Wakongwe hao walianza mechi yao taratibu wakishambuliana kwa zamu na kumaliza kipindi cha kwanza suluhu.
Simba ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 57 ambapo mchezaji wake Shiza Kichuya alifunga akiunganisha pasi ya John Bocco aliyeingia dakika ya 56 kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo.
Bao hilo lilidumu kwa dakika tatu tu kabla Obrey Chirwa hajaisawazishia Yanga akiunganisha pasi ya Geofrey Mwashiuya.
Mechi ya jana haikuwa na shangwe nyingi kama ilivyo kawaida ya mechi za watani pengine ni kutokana na uchache wa watu waliofika uwanjani hapo kushudia mechi hiyo, tofauti na ilivyozoeleka mechi hiyo hujaza mashabiki wengi.
Aidha, muda mwingi wa mchezo wachezaji wa timu zote walionekana kucheza kwa kujilinda zaidi.
Dakika ya 22 Emmanuel Okwi alipata nafasi nzuri ya kufunga lakini mpira wake wa kichwa ulitoka nje ya goli.
Dakika moja baadaye nusura Mwashiuya aipatie Yanga bao lakini mpira wake wa kichwa ulipaa nje.
Simba ilipata tena nafasi katika dakika ya 27 ambapo mshambuliaji wake Mrundi Laudit Mavugo alishindwa kufunga baada ya shuti lake kutoka pembeni ya goli.
Dakika ya 32 Chirwa alikokota mpira mpaka kwenye boksi lakini akashindwa kufunga na mpira kupita pembeni ya goli.
Sare hiyo inairudisha Simba kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa uwiano mzuri wa mabao, huku Yanga ikishika nafasi ya pili na Azam ya tatu. Zote zina pointi 16.
Yanga: Youthe Rostand, Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vicent, Kelvin Yondani, Papy Tshitshimbi, Pius Buswita, Raphael Daud/ Pato Ngonyani, Obrey Chirwa,Ibrahim Ajibu, Geofrey Mwashiuya/ Emmanuel Martin
Simba: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jnr’, Juuko Murshid, Method Mwanjale, James Kotei/ Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Muzamiru Yassin/ Said Ndemla, Laudit Mavugo/ John Bocco, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima.

Saturday, October 28, 2017

MAN UNITED vs TOTTENHAM HOTSPUR NANI KUIBUKA KIDEDEA?

Image result for MAN UNITED VS SPURS

SIMBA NA YANGA KUONESHANA KAZI KATIKA UWANJA WA UHURU PUNDE LEO


MACHO na masikio ya mashabiki wa soka leo yataelekezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam pale watani wa jadi, Yanga na Simba watakapomenyana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mashabiki wa timu hizo wamekuwa wakitambiana kuanzia mitaani, nyumbani, katika vyombo vya usafiri, sokoni, vijiweni na kila mahali, ambapo kila mmoja akitamba kuibuka na ushindi leo.


UPINZANI MKALI
Upinzani mkali kwa timu hizo unaonekana kuongezeka baada ya Yanga kumchukua mshambuliaji hatari wa watani wao wa jadi Simba, Ibrahim Ajibu, huku Simba nao wakimchukua Haruna Niyonzima.

Wawili hao hasa Ajibu ameonesha makali na kuisaidia Yanga kupata mabao kibao, huku mchezaji huyo naye akiwania kiatu cha dhahabu kama alivyo Emmanuel Okwi wa Simba.
Ushindani mkali utakuwa kwa Ajibu na Okwi katika mbio za kupachika mabao, kwani wachezaji hao wameonesha makali yao karibu katika kila mchezo wa timu zao walizocheza.
Katika msimamo wa ufungaji, Okwi anaongoza akiwa na mabao nane na amekuwa tegemeo kubwa kwa timu yake ya Simba, hasa katika mechi zinazowakutanisha na Yanga, kwani ana rekodi nzuri ya kuwafunga wapinzani hao.


Pia Okwi amefunga katika michezo yote ya Ligi Kuu aliyocheza msimu huu hususani kwenye Uwanja wa Uhuru, ambao ndio utakaotumika kuchezewa mchezo huo wa leo.
Ajib katika msimamo wa ligi tayari ameshafunga mabao matano na ndiye mchezaji anayeongoza kwa mabao kwa Yanga na hakuna ubishi kuwa mchezaji huyo yuko katika kiwango cha juu cha uchezaji katika kipindi hiki huku akiwafunika Tambwe na Ngoma
Hivyo, kulingana na ubora wa wachezaji hao wawili ni sababu mojawapo kubwa baina timu hizi na wanatarajiwa kuwa nguzo katika mchezo huo wa aina yake na pengine kuwa na upinzani wa juu zaidi.


Mchezo wa watani wa jadi mara kadhaa wachezaji wanalaumiwa pindi timu moja inapopoteza mchezo, makocha kufukuzwa pia viongozi hushambuliwa kwa maneno makali na mtaani mashabiki wanataniana na ukiwa una hasira za karibu unaweza kujikuta unarusha ngumi kwa sababu ya hizi timu mbili.
Katika michezo saba iliyopita ya Ligi Kuu Tanzania Bara zilizokutana tangu mwaka 2014 hadi 2017, Simba imeshinda michezo miwili na Yanga imeshinda miwili na kutoka sare mitatu.


Matokeo ya mechi Yanga na Simba

28/10/2017 Yanga ?? Simba
25/02/2017 Simba 2-1 Yanga
01/10/2016 Yanga 1-1 Simba
20/02/2016 Yanga 2-0 Simba
26/09/2015 Simba 0-2 Yanga
08/03/2015 Simba 1-0 Yanga
18/10/2014 Yanga 0-0 Simba
19/04/2014 Yanga 1-1 Simba



REKODI ZA MAKOCHA

Kwa upande wa makocha, George Lwandamina hajawahi kuifunga Simba, hivyo rekodi inambeba Omog wa Simba ambaye ameiongoza timu hiyo kuifunga Yanga katika mechi nne.



Mechi ya kwanza Omog ilikuwa Oktoba mwaka jana katika mchezo wa Ligi Kuu, ambapo aliiongoza Simba kupata sare ya bao 1-1 licha ya timu yake kuwa pungufu uwanjani baada ya kiungo Jonas Mkude kupewa kadi nyekundu na baadaye bao la kona ya winga Shiza Kichuya kumuokoa dakika za majeruhi.


Mchezo uliofuata wa Ligi Kuu ulikuwa Februari, ambapo aliibuka na ushindi wa mabao 2-1 licha ya timu yake kubaki tena pungufu uwanjani baada ya beki Besala Bokungu kutolewa kwa kadi nyekundu.

Mechi nyingine mbili alizocheza bila kufungwa na Yanga ni ule wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi aliposhinda kwa penalti 4-3 pamoja na mchezo wa Ngao ya Jamii wa Agosti mwaka huu akishinda kwa penalti baada ya suluhu katika dakika 90.

Swali linabaki Omog atafanikiwa kulinda rekodi yake mbele ya Yanga kwa kuibana na kushinda au kutoa sare au atashindwa kulinda na kupokea kipigo kwa mara ya kwanza tangu aanze kuinoa timu hiyo?
Katika kujiandaa na mchezo huu timu zote ziliweka kambi nje ya Dar es Salaam wakati Yanga wakiwa Morogoro, Simba ilipanda ndege hadi visiwa vya Zanzibar na wote walitarajia kurejea jana tayari kwa mchezo huo.

Tusubiri baada ya dakika 90 nini kitatokea katika mchezo huo maarufu kama Kariakoo `Derby’ ambayo ni miongoni mwa mechi kubwa tatu barani Afrika baada ya ‘Cairo Derby’ ambayo huzihusisha timu pinzani nchini Misri, Al Ahly dhidi ya Zamalek na ‘Soweto Derby’ inayohusisha timu za Orlando Pirates dhidi ya Kaizer Chiefs zote za Afrika Kusini.
 

MAKOCHA KUTIMULIWA
Mechi za Yanga na Simba zimekuwa balaa kwa makocha, kwani wakati mwingine wanajikuta wakitimuliwa kutokana na matokeo ya uwanjani kutokuwa mazuri kwa timu zao.

Hata hivyo, katika mchezo wa leo, Omog ndiye anayeonekana kuwa katika hatari zaidi ya kutupiwa virago endapo atafungwa, kwani tayari uongozi wa timu hiyo ulishawahi kumchimba mkwara kwa matokeo mabaya ya nyuma.

Tayari Simba wameshamleta nchini aliyekuwa kocha Mkuu wa Rayon Sports, Djuma Masoud kumsaidia Omog na ndiye alikuwa kocha bora wa Ligi ya Rwanda msimu uliopita, huenda akachukua Mcameroun endapo atatupiwa virago.

Kocha Omog pamoja na kukibadilisha kikosi chake na kucheza kandanda safi bado uongozi unaonesha wakati fulani kutoridhika na matokeo hayo.
Kwa upande wa Mzambia George Lwandamina wa Yanga, yeye anaonekana hayuko hatari sana kwani Yanga wameonesha kumkubali na hivyo wako tayari kumvumilia aendelee kuwepo katika kikosi chao.

Hata hivyo, uongozi na mashabiki wa timu hizo mbili huwa hawana msamaha pale wanapoona timu yao imefanywa 'kitu mbaya' na wapinzani wao wa jadi na kuwakosesha usingizi.

Viingilio katika mchezo huo vitakuwa Sh 10,000 kwa mzunguko wakati 20,000 ni kwa jukwaa kuu.

SANGA ATEUA WAJUMBE 12 KAMATI YA LIGI

MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga ameteua wajumbe 12 akiwemo yeye mwenyewe watakaounda kamati ya bodi ya ligi katika kikao kilichofanyika juzi.
Katika taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari na Boniface Wambura ambaye ndiye Katibu wa kamati hiyo inasema kamati itashughulikia uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili
“Kamati itaongozwa na Mwenyekiti mwenyewe, Shani Mligo ambaye ni Makamu Mwenyekiti, Boniface Wambura ambaye ni Katibu, wajumbe ni Issa Batenga, Leslie Liunda na Wakili Saleh Njaa,” alisema Wambura.
Wengine ni Dk. Ellyson Maeja, George Malawa, Isaac Chanji, Baruan Muhuza, Mbakileki Mutahaba na Ally Mayay.
Pia Sanga amewateua Kanali Charles Mbuge ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Ruvu Shooting, na Abuu Changawa (Majeki) kuingia kwenye kamati ya uongozi ya TPLB kwa mujibu wa Ibara ya 28(vi) ya Kanuni za Uendeshaji za TPLB ambayo inampa nafasi ya kuteua wajumbe wawili

Tigo yazindua mbio za Kili Half Marathon 2018


Kaimu mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo akijitambulisha wakati wa kuzindua mbio za Kili Half Marathon kwa mwaka 2018, mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Kili Marathon kwa mwaka 2018, uzinduzi huo umefanyika jana jijini Dar es Salaam ambapo kampuni ya simu za mkononi ya Tigo itadhamini mbio za kilomita 21 kwa jina la Tigo Kili Half Marathon.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mbio za Kili Marathon kwa mwaka 2018, uzinduzi huo umefanyika jana jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo ambao wamedhamini mbio za kilomita 21 ziitwazo Tigo Kili Half Marathon

DR MWAKYEMBE AZINDUA KILIMANJARO MARATHON


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dk Harrison Mwakyembe (katikati), akikata utepe kuzindua rasmi mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 Dar es Salaam. Wengine kutoka (kushoto) ni Meneja Masoko wa TBL Group anayesimamia Grand Malt, Warda Kimaro, Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo, Alex Nkenyenge, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis na Makamu wa Rais wa Chama Cha Riadha Tanzania, William Kallaghe.

Washindi wa Vipaji vya Sauti lafikia tamati jijini Dar, Kumi kwenda China


Washindi 25 wa shindano la vipaji vya sauti wakiwa kwenye fainali hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.

Msanii maarufu nchini Tanzania Kutoka kundi la Orijino Komedi maarufu kama Mpoki a k a Muarabu wa Dubai(wa kwanza kulia) kizungumza jambo mara baada ya kutaja washindi 25 waliofuzu kuingia fainali ya shindano la Vipaji vya Sauti katika tamthiliya za kigeni kwa awamu ya pili ya mwaka 2017.
Majajji wa shindano la vipaji vya sauti la awamu ya pili lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kishoto ni Msanii wa filamu nchini Jacob Stephen maarufu kama JB, kulia Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto pamoja na aliyekuwa mshindi wa shindano la vipaji vya sauti mwaka 2016/17.






Baadhi ya washiriki wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili wa mshindano hayo yanayodhamuniwa na Startimes Tanzania wakionesha namna wanavyoweza kuigiza sauti kwenye fainali iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Msanii maarufu nchini Tanzania Kutoka kundi la Orijino Komedi maarufu kama Mpoki a k a Muarabu wa Dubai akizungumza jambo kwenye fainali ya shindano la kusaka vipaji lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili kwa mwaka 2017.

Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif akizungumza na waandishi wa habari wakati wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili mwaka 2017 lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.

Washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti walioshinda kwenda nchini China kufanya kazi makao makuu ya Kampuni ya Startimes kwenye fainali hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa washindi walioingia kumi bora akipokea zawadi ya simu ya Startimes kutoka kwa Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif mara baada ya kumalizika kwa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi(kulia) akimkabidhi zawadi ya Television ya Startimes mshindi wa kwanza wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili, Coletha Raymond mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.




Mshindi wa kwanza hadi wa tatu wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili mwaka 2017 wakiwa kwenye picha ya Pamoja.

Wednesday, October 25, 2017

MANCHESTER UNITED YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CARABAO KWA KUICHAPA KIULAINI BAO 2-0 SWANSEA CITY


Mabingwa watetezi wa kombe la Carabao Manchester United wametinga robo fainali ya michuano hiyo kiulaini kwa kupata ushindi mwepesi wa magoli 2-0 dhidi ya Swansea City. Kikosi cha Manchester United kilichofanyiwa mabadiliko makubwa kiliutawala mchezo huo na kupata goli la kwanza kupitia kwa Jesse Lingard kufuatia pande la kisigino la Marcus Rashford.

Wageni Manchester United waliongeza goli la pili kwa shambulizi zuri ambapo mpira ulimkuta Lingard na kufunga kwa mpira wa kichwa.


Jesse Lingard akipiga mpira uliozaa goli la kwanza la Manchester United

Mshambuliaji Marcus Rashford akiwatoka wachezaji wa Swansea City

KIPA CLAUDIO BRAVO APANGUA PENATI NA KUIPELEKA MAN CITY ROBO FAINALI


Kipa Claudio Bravo ameibuka kuwa shujaa wa Manchester City katika mchezo wa jana dhidi ya Wolves baada ya kupangua mikwaju ya penati na kutinga robo fainali ya kombe la Carabao.
Bravo, aliyeokoa michomo mitatu katika muda wa kawaida aliongeza kuonyesha ushujaa wake kwa kupangua penati za Alfred N'Diaye na Conor Coady baada ya mchezo kuisha kwa sare tasa.

Manchester City ilifunga penati zote nne huku, Sergio Aguero akimalizia kiufundi penati ya nne na kufanya matokeo kuwa 4-1.


Kipa wa Manchester City Claudio Bravo akipangua penati ya Alfred N'Diaye

Sergio Aguero akishangilia baada ya kutumbukiza golini mpira wa penati

Tuesday, October 24, 2017

RONALDO, MESSI NA NEYMAR WAUNDA KIKOSI CHA WACHEZAJI 11 BORA DUNIA

Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar wametajwa katika kikosi bora cha wachezaji 11 wa Shirikisho la Soka la Fifa.
Ronaldo ameungana katika orodha hiyo na nyota wenzake wa Real Madrid ambao ni Marcelo, Sergio Ramos, Luka Modric pamoja na Toni Kroos.
Kipa Gianluigi Buffon, aliyetwaa tuzo ya kipa bora wa Fifa naye yumo katika kikosi hicho, huku Dani Alves, Andres Iniesta na Leonardo Bonucci wakikamilisha kikosi hicho.


Wachezaji wa kikosi Bora cha Wachezaji 11 wa Fifa wakipiga picha na mshereheshaji Idris Elba ambaye ni muigizaji nyota wa filamu

RONALDO ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA SOKA DUNIANI


Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa mchezaji bora soka wa kiume kwa mwaka 2017 na Shirikisho la Soka la Dunia FIFA Jijini London.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid na Ureno amemshinda Lionel Messi wa Barcelona na Neymar wa Paris St-Germain.
Ronaldo, 32, aliisaidia Real Madrid kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na ubingwa wa La Liga.


Cristiano Ronaldo akishukuru kwa tuzo huku akiangaliwa na Diego Maradona pamoja na Ronaldo de Lima

Cristiano Ronaldo akiwa na tuzo yake pamoja na kocha wake Zinedine Zidane aliyeshinda tuzo ya kocha bora