Na Faustine Ruta, Bukoba
Kikosi cha Timu ya Simba kimefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, yakiwa ni maandalizi ya kukabiliana na kikosi cha Timu ya Kagera shugar hapo kesho jioni.
Kikosi hicho ambacho kinaongozwa na Kocha Masoud Djuma ambacho kilitua katika ardhi ya Kagera siku ya Ijumaa kimefanya mazoezi ya mwisho katika dimba la Kaitaba, huku kocha wa kikosi hicho akisema mechi yao na Kagera sugar itakayopigwa hapo kesho inahitaji nidhamu ya hali ya juu ili kuweza kuibuka kidedea.
Kagera sugar wanakutana na Simba wakiwa na taadhali kubwa baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Njombe mji huku Simba wakiwaadabisha matajiri wa Arizeti Singida United kwa mabao 4-0 wiki hii.
Katika mazoezi ya hayo kocha wa timu ya Kagera Sugar Mecky Meckime amezungumzia maandalizi ya mchezo huo na kueleza kuwa kikosi chake kiko imara licha ya kutokuwa na matokeo mazuri tangu Ligi hii ianze msimu 2017/2018.


No comments:
Post a Comment