
Timu ya Arsenal imeifanyia kitu mbaya Everton kwa kuichakaza kwa magoli 5-1 huku Aaron Ramsey akitupia hat-trick katika mchezo ambao timu hiyo inayonolewa na kocha Arsene Wenger ikionyesha kuimarika.
Katika mchezo huo Wenger pia alishuhudia mchezaji wake mpya aliyemnunua kwa bei mbaya Pierre-Emerick Aubameyang akifunga goli katika mchezo wake wa kwanza akipatiwa pande mgeni mwenzake Henrikh Mkhitaryan.
Katika mchezo huo Aaron Ramsey alifunga hat-trick yake ya kwanza kwa kucheka na nyavu katika dakika 6, 19 na 74 za mchezo huo huku naye Laurent Koscielny alifumania nyavu kwa kufunga goli la pili.

Aaron Ramsey akifunga goli kati ya magoli yake matatu aliyoyafunga hapo jana

Pierre-Emerick Aubameyang akifunga goli lake la kwanza akiwa na Arsenal kwa mpira wa kuubetua juu ya kipa
No comments:
Post a Comment