Sanchez leo ameifungia bao kwa mkwaju wa penati Man United na kufanya mtanange kipindi cha pili kubadilisha matokeo na kuumaliza kwa bao 2-0 dhidi ya Timu ya iliyopanda Daraja msimu huu 2017/18 ya Huddersfield. Bao la kwanza lilifungwa na Lukaku dakika ya 55 na bao la pili akafunga Sanchez kwa mkwaju wa penati dakika ya 60. kwa matokeo hayo Man United wamebaki nafasi ya pili wakiwa na alama 56 huku kileleni akisimama Man City mwenye alama 69.
Sanchez akipongezwa na Paul Pogba aliyeingia kipindi cha pili
Romelu Lukaku akitupia kambani dakika ya 55
Lukaku alipata pasi kutoka kwa Juan Mata na kufunga bao hilo kipindi cha pili
Lukaku akipongezwa na Jesse Lingard pamoja na Alexis Sanchez
No comments:
Post a Comment