Kocha Mauricio Pochettino ameipongeza Tottenham kwa kupambana kishujaa na kupata goli ndani ya sekunde 11 la Christian Eriksen lililosaidia ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Manchester United katika dimba la Wembley.
Baada ya goli hilo Manchester United walijaribu kutaka kusawazisha huku Jesse Lingard akikosa goli, lakini Phil Jones alizamisha jahazi baada ya kujifunga la pili akitumbukiza krosi ya
Kieran Trippier.

Christian Eriksen akifunga goli la kwanza ndani ya sekunde 11 tu ya mchezo

Bournemouth ilipata magoli yake hayo katika kipindi cha pili kupitia kwa Callum Wilson, Junior Stanislas na Nathan Ake na kuipatia timu hiyo ushindi wake wa kwanza wa ugenini katika michezo saba.

Alexis Sanchez akiteta jambo na Martial
No comments:
Post a Comment