BUKOBA SPORTS

Thursday, February 1, 2018

MANCHESTER CITY HAISHIKIKI LIGI KUU UINGEREZA, YAIBAMIZA BAO 3-0 WEST BROM


Manchester City imekwea kwa tofauti ya pointi 15 kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuifundisha soka West Brom katika dimba la Etihad Stadium na kuibuka na ushindi wa magoli 3 bila majibu.
Fernandinho alitangulia kufunga goli la kwanza kwa pande la Kevin de Bruyne goli lililodumu katika kipindi cha kwanza kisha De Bruyne na kisha baadaye Sergio Aguero akaongeza goli la tatu.


Fernandinho akifunga goli la kwanza katika mchezo huo

Kocha wa Everton Sam Allardyce amesema mchezaji wake mpya Theo Walcott ameanza kulipa gharama walizoingia baada ya kufunga magoli mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Leicester.

Walcott, akiichezea Everton kwa mara ya pili tangu ajiunge nayo kwa ada ya paundi milioni 20, ameisaidia timu hiyo kupata ushindi wa nane katika michuano yote.

Mchezaji mpya wa Everton Theo Walcott akifunga goli la kwanza katika mchezo huo

No comments:

Post a Comment