BUKOBA SPORTS

Sunday, February 18, 2018

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA ASHUHUDIA MECHI KATI YA KAGERA SUGAR v SINGIDA UNITED, KAITABA MJINI BUKOBA



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akisalimiana na viongozi muda mfupi kabla ya kipute hicho kuanza cha Wakata miwa Kagera Sugar vs Singida United. Kagera Sugar ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Singida United.

Timu zikiingia Uwanjani

Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya Kagera Sugar ndio ilipata bao ikiwa ya kwanza kupitia kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Singida United Michael Rusheshangoga kuunawa ndani ya 18, Mkwaju uliopigwa na Beki wa Kagera Sugar Mohammed Fakhi dakika ya 34. Kipindi cha pili Singida United walirudi na nguvu na kufanikiwa kuiteka ngome ya Kagera Sugar na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha mapema kipindi cha pili dakika ya 49 kupitia kwa Kambale Salita.

Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar kilichoanza

Kikosi cha Timu ya Singida United kilichoanza dhidi ya Timu ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba leo.
Picha na Faustine Ruta, BukobaWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) (katikati) akishuhudia mtanange huo kwenye Uwanja wa Kaitaba. Kagera Sugar wametoshana nguvu na Singida United. Picha na Faustine Ruta, Bukoba

No comments:

Post a Comment