Tuesday, May 29, 2018

SIMBA WALIVYOKABIDHIWA MWALI WAO

MABINGWA wapya wa Ligi Kuu Bara Simba,jana walikabidhiwa ubingwa wao na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuri katika uwanja wa Taifa Dar es saam.
Simba walitwaa ubingwa huo,licha ya kupoteza mchezo wake wa kwanza kwa bao 1-0 mbele ya Magufuri,hivyo kuvunjia rekodi yake ya kutopoteza mchezo katika Ligi hiyo.
Mshambuliaji Edward Christopher ndiye aliyefunga bao hilo wakati mpira ukielekea ukingoni kunako dakika ya 85,kabla ya Simba kupata penalti dakika ya 93 iliyopigwa na Emmanuel Okwi na Juma Kaseja kupangua.
Aidha,Mgeni rasmi wa mchezo huo,Rais Magufuri aliwapongeza Simba kwa kutwaa ubingwa huo na kuwasihi kuendelea kupambana ikibidi watwae ubingwa wa Afrika.
Akizungumza kabla ya kukabidhi ubingwa huo,alisema Mabingwa hao walistahili kuchukua ubingwa huo,kutokana na namna walivyopambana,lakini hakusita kuipongeza Kagera Sugar kwa kuonesha mchezo mzuri.
Magufuri aliipongeza Wizara husika na uwongozi wa TFF kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kuifanya katika kuhakikisha mpira wa Tanzania unakuwa kila siku.
Pia alizungumzia ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa katika Jiji la Dodoma,ambapo alisema Serikali ipo katika mchakato huo na kuongeza matukio ya ajabu kama kung’oa viti hayapaswi kujirudia tena.




Ameziomba Halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanja na kuomba visimamiwe kwa ubora wa hali ya juu kuhakikisha havivamiwi na mtu yoyote.
Naye,Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe, alisema uwanja wa Taifa ndiyo utakaotumika katika michuano ya AFCON kwa vijana wenye umri wa miaka 17 itakayofanyika mwakani katika ardhi ya nyumbani. Alisema uwanja huo na ule wa uhuru,vinahitaji marekebisho ya hali ya juu ili kuviweka sawa kabla ya michuano hiyo kuanza mwezi Aprili 2019.

No comments:

Post a Comment