BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 10, 2012

NASRI AIKANDYA ARSENAL

Samir Nasri ameshikilia msimamo wake alioutabiri mwanzoni mwa Msimu kwamba Manchester City watatwaa Kikombe kabla Arsenal kumaliza ukame wao wa Makombe uliodumu Miaka 7 sasa.
Wakati akiihama Arsenal mwanzoni mwa Msimu, Nasri alitamba kuwa anaenda Man City ili kutwaa Ubingwa ingawa baadhi ya Wadau walimnanga kwa kudai ameenda huko kufuata fedha tu.

Lakini, baada ya juzi Man City kuchapwa 1-0 na Arsenal na kuwaacha wakiwa Pointi 8 nyuma ya vinara Man United huku Mechi zimebaki 6, yale matumaini ya Nasri ya kutwaa Ubingwa yanaelekea kufifia kama si kuzimika kabisa.

Hilo limeshikiwa bango na Mashabiki wa Arsenal ambao wamemjibu Nasri na kumkumbusha kauli yake na pia kumpasha kuwa na yeye atamaliza Msimu huu akiwa mikono mitupu.

Hata hivyo Nasri amejibu mapigo kwenye mtandao wa Twitter alipoposti: ‘Najua nini nilisema kuhusu Mataji. Nina hakika City watabeba Kombe kabla Arsenal. Na kwa Mashabiki wote wa Arsenal, acheni! City wako Pointi 10 mbele yenu. Nyie sapoti Timu yenu na muachane na mimi.’

No comments:

Post a Comment