Brendan Rodgers, Miaka 38, ambaye ni Meneja wa Swansea City, amekubali kuwa Meneja mpya wa Liverpool na anatarajiwa kusaini Mkataba wa Miaka mitatu ndani ya Masaa 24 yajayo.
Kwa kumchukua Rodgers, Liverpool itabidi wawalipe Swansea City fidia ya kati ya Pauni Milioni 4 hadi 5.

Liverpool walimtimua Meneja wao Kenny Dalglish hapo Mei 16 baada ya kumaliza nafasi ya 8 kwenye Ligi Kuu England Msimu huu uliomalizika majuzi ingawa alimudu kubeba Carling Cup na kuifikisha Liverpool Fanali ya FA Cup ambayo walifungwa na Chelsea.

Liverpool walimtimua Meneja wao Kenny Dalglish hapo Mei 16 baada ya kumaliza nafasi ya 8 kwenye Ligi Kuu England Msimu huu uliomalizika majuzi ingawa alimudu kubeba Carling Cup na kuifikisha Liverpool Fanali ya FA Cup ambayo walifungwa na Chelsea.
Rodgers, Msimu huu, alimudu kuiwezesha Swansea kumaliza nafasi ya 11 na iliwafunga Liverpool bao 1-0 kwenye Mechi ya mwisho ya Ligi.
Uteuzi wa Rodgers umeshangaza maana muda wote ilitegemewa Meneja wa Wigan, Roberto Martinez, ndiye ambaye angelitwaa wadhifa huo na juzi Mwenyekiti wa Wigan, Dave Whelan, alitangaza Liverpool imeshampa ofa Martinez.
KUHUSU BRENDAN ROGERS!
•1973: Alizaliwa Januari 26 huko Carnlough, Northern Ireland
•1987: Alianza Soka kama Beki na Ballymena United
•1990: Ajiunga na Reading kama Chipukizi lakini akalazimika kustaafu baada ya kuumia. Alibaki hapo kama Kocha
•2004: Jose Mourinho amteua Rodgers kama Kocha Timu ya Vijana Chelsea
•2006: Apewa promosheni Chelsea na kuwa Kocha wa Timu ya Rizevu
•2008: Ajiunga na Watford
•Juni 2009: Arudi tena Reading kuwa Meneja badala ya Steve Coppell
•Desemba 2009: Aondoka Reading baada ya matokeo mabovu
•Julai 2010: Ajiunga na Swansea
•Mei 2011: Aipandisha Swansea Ligi Kuu
•Mei 2012: Aliifikisha Swansea kumaliza nafasi ya 11 Ligi Kuu
No comments:
Post a Comment