BUKOBA SPORTS

Thursday, May 31, 2012

KILA KWENYE WATU KUMI, MMOJA NI SHABIKI WA MASHETANI WEKUNDU MAN UNITED!

Manchester United imedai kwamba inamiliku zaidi ya sailimia 10 ya mashabiki wote wa soka Duniani kote.
united ilitangaza juzi kwamba kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa, zimeonyesha kwamba miamba hiyo ya Old Traford imeweza kukusanya zaidi ya mabao milioni 659 katika kipindi cha miaka mitano.(5) Idadi hiyo  ni karibu moja ya 10 katika watu bilioni saba waliopo ulimwenguni.
                                         KWENYE MIAKA YA    (1969-1986)
;
Kufuatia utafiti uliofanywa na Wakala wa Utafiti wa Masoko, Kantar, ambao ni moja wa vinara wa fani hiyo, uliofanywa katika Nchi 39, Manchester United ndio imetangazwa kuwa ni Klabu ya Soka inayoongoza Duniani kwa kupendwa baada ya kubainishwa na Mashabiki Milioni 659 katika utafiti huo kuwa ndio Klabu wanayoipenda.
 
Hivi karibuni, Mtandao wa Forbes, ambao ni Magwiji wa masuala ya Biashara na Fedha Duniani, waliitangaza Man United kuwa ndio Klabu yenye thamani, kifedha kupita Klabu yeyote Duniani.
 
Kantar pia imegundua kuwa Soka ndio Mchezo unaopendwa zaidi kupita yote ukiwa na Mashabiki Bilioni
1.6 na takwimu hizo zinalingana na utafiti uliofanywa na FIFA hivi karibuni.
 
Akiongelea kuhusu mikakati ya muda mrefu ya Klabu ya Manchester United, Mkurugenzi wa Biashara wa Klabu hiyo, Richard Arnold, amesema: ‘‘Man United imejenga utamaduni wa kuwa na Wachezaji Nguli, Timu Bora na mafanikio makubwa Beckham, Busby, Benfica Mwaka 1968! Sasa hivi Mechi zetu zinatangazwa na kufuatiliwa katika kaya zaidi ya Bilioni 1.15 Dunia nzima na kwa Mwaka zaidi ya Bilioni 4!’
"Mkurugenzi huyo alimalizia kwa kusema Familia ya Washabiki wao inakuwa Siku hadi Siku."

Manchester United ina Mashabiki Milioni 659 Duniani kote:
- Milioni 71 Marekani

- Milioni 90 Ulaya

- Milioni 173 Afrika na Mashariki ya Kati

- Milioni 325 Asia

No comments:

Post a Comment