BUKOBA SPORTS

Thursday, May 31, 2012

DENNIS OLIECH AJIRUDISHA KUNDINI BAADA YA MGOMO WA KUIGOMEA HARAMBEE STARS YA KENYA!

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Kenya, Dennis Oliech, amebadili uamuzi wake wa kutoichezea Nchi yake baada ya kufarakana na Shirikisho la Soka Kenya, FKF, kuhusu Wachezaji kustahili mgao unaotokana na udhamini wa Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki, East African Breweries Limited.
Shirikisho la Soka Kenya, FKF, lilidai Mchezaji huyo hakuwa na haki hiyo kwa vile hamna kipengele hicho kwenye Mkataba na Mdhamini.

Oliech, anaecheza Klabu ya Ufaransa Auxerre ambayo Msimu huu imeporomoka Daraja, ataiongoza tena Nchi yake kwenye Mechi ya Mchujo ya KUNDI F dhidi ya Malawi hapo Jumamosi Juni 2 Mjini Nairobi ili kutafuta kuingia Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 zitazochezwa Brazil.
 

Wakati wa mgogoro wa Oliech na FKF, Mwenyekiti wa FKF, Sam Nyamweya, alisema: ‘Mkataba unawaruhusu Wadhamini kutumia picha za Timu ya Taifa katika matangazo. Lakini sasa tunaongea nao upya ili nao Wachezaji wanufaike.’

Mechi inayofuata ya Kenya ya KUNDI F ni ugenini huko Windhoek dhidi ya Namibia.


KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014 = KANDA YA AFRIKA

MAKUNDI:

KUNDI A=Ethiopia,Central Africa Republic, Botswana, South Africa

KUNDI B = Equatorial Guinea, Sierra Leone, Cape Verde, Tunisia

KUNDI C = Tanzania, Gambia, Morocco, Ivory Coast

KUNDI D = Lesotho, Ghana, Sudan, Zambia

KUNDI E = Congo, Burkina Faso, Niger, Gabon

KUNDI F = Namibia, Kenya, Malawi, Nigeria

KUNDI G = Mozambique, Zimbabwe, Guinea, Egypt

KUNDI H = Rwanda, Algeria, Benin, Mali

KUNDI I = Congo DR, Togo, Libya, Cameroun

KUNDI J = Liberia, Angola, Uganda, Senegal


RATIBA
RAUNDI MBILI ZA MWANZO

Ijumaa Juni 1

Zimbabwe v Guinea

Angola v Uganda

Ghana v Lesotho

Egypt v Mozambique

Jumamosi Juni 2

Togo v Libya

Kenya v Malawi

Central African Republic v Botswana

Cameroon v Congo, DR

Sierra Leone v Cape Verde

Gambia v Morocco

Sudan v Zambia

Tunisia v Equatorial Guinea

Ivory Coast v Tanzania

Burkina Faso v Congo

Senegal v Liberia

Algeria v Rwanda

Jumapili Juni 3

South Africa v Ethiopia

Niger v Gabon

Benin v Mali

Nigeria v Namibia

Ijumaa Juni 8

[FAHAMU: Baadhi ya Mechi zitachezwa Jumamosi na Jumapili. Tutajulisha baadae]

Botswana v South Africa

Ethiopia v Central African Republic

Equatorial Guinea v Sierra Leone

Cape Verde v Tunisia

Morocco v Ivory Coast

Tanzania v Gambia

Lesotho v Sudan

Zambia v Ghana

Congo v Niger

Gabon v Burkina Faso

Malawi v Nigeria

Namibia v Kenya

Guinea v Egypt

Mozambique v Zimbabwe

Rwanda v Benin

Mali v Algeria

Libya v Cameroon

Congo, DR vTogo

Uganda v Senegal

Liberia v Angola

No comments:

Post a Comment