BUKOBA SPORTS

Thursday, May 31, 2012

SERIKALI YACHANGIA MILIONI 10 KAMA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU KANUMBA


Tunafarijika sana sisi wasanii na serikali yetu ya sasa hatuna cha kuwapa zaidi ya shukrani zetu za dhati kwenu kwa kipaumbele mnachotupatia kwa sasa hii haijawahi kutokea katika serikali zote zilizopita tunakushukuru sana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kututhamini sisi wasanii wa Tanzania, kwanini nasema hivi leo.., serikali yetu ya Tanzania imetoa milioni kumi kwa famila ya marehemu Steven Kanumba kama rambirambi ya serikali yetu. Familia ya The Great na sisi wasanii wote Bongo Movie tunasema tunawashukuru sana..

Naibu Waziri wa utamaduni na michezo Mhe, Amos Makalla akiwa anawasili nyumbani kwa marehemu Kanumba kwa ajili ya kutoa rambirambi hiyo sisi wasanii tunasemaje Mhe.Amosi Makala ni chaguo sahihi katika wizara aliyopewa tunampenda sana maana anajali sana wasanii

Mheshimiwa akiwa makini kufuatiliia ratiba zinazoendelea..

Mama wa marehemu akiwa na Mh; Amos Makalla.
Mh; akiwa ameshika kiasi cha milioni kumi(mil 10) kwa ajili ya kukabidhi kwa familia ya marehemu kama rambi rambi ikimwakilisha Mh. Rais Jakaya Kikwete na Serikali yake.

Kabla ya kukabidhiana mama aliongea machache na kutoa shukrani zake kwa serikali..

Makabidhiano yakafanyika.

Mama akipokea pesa hizo kwa majonzi makubwa

Mama wa marehemu akionyesha kiasi cha fedha alichokabidhiwa kwa niaba ya ndugu na jamaa waliokuwepo

Mama akisaini mkataba toka kwa mwanasheria wa Wizara habari utamaduni na michezo

Seth(Mdogo wa marehemu) naye pia alisaini kama shaidi.

No comments:

Post a Comment