BUKOBA SPORTS

Saturday, May 12, 2012

POLISI YALINDA USALAMA KATIKA KLABU YA YANGA JANGWANI

Baadhi ya wanachama wa Yanga wakifanya fujo klabuni hapo kupinga mkutano wa waandishi wa habari uliokuwa ufanywe na mwenyekiti wa klabu hiyo Bw. Loyd Nchunga jana  mchana ambapo polisi walifika klabuni hapo na kuimarisha ulinzi. Mpaka  mwakilishi wa bukobasports.com  anaondoka klabuni hapo bado kulikuwa na kundi la wanachama na kila mmoja akiongea la kwake na mkutano ulikuwa bado kufanyika.
 Mmoja wa askari akimuondoa mmoja wa wanachama wa klabu hiyo katika eneo lililokuwa na vurugu klabuni hapo.
Polisi wakiwa katika magari yao tayari kabisa kuzuia vurugu endapo zingezuka klabuni hapo.
Moja wa magari ya polisi likiwa limeegeshwa nje ya klabu hiyo kwa ajili ya kulinda usalama klabuni hapo leo mchana

No comments:

Post a Comment