BUKOBA SPORTS

Thursday, June 14, 2012

Di MATTEO SASA MENEJA WA KUDUMU CHELSEA, ASAINI MIAKA MIWILI!

Chelsea hatimaye imemteua Roberto Di Matteo kama meneja wake wa kudumu kwa kutiliana saini mkataba wa miaka miwili.
Di Matteo aliwekwa kama kocha wa mda kufuatia kutimuliwa kwa Andre Villas-Boas mnamo mwezi Machi, na akaweza kuiongoza klabu hio akifanikiwa kuifikisha na kushinda fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na vilevile kombe la FA la England.
 
Meneja huyo aliyekua kiongozi wa MK Dons na pia West Brom, Di Matteo alipoteza mechi tatu tu kati ya mechi 21 alizosimamia, na kutokana na hali hiyo wachezaji wengi wa klabu waliunga mkono ateuliwe kama meneja wa kudumu hususan baada ya kushinda kombe lililoikwepa klabu hio kwa mda mrefu la Mabingwa wa Ulaya.

MAMENEJA WA CHELSEA TANGU ABRAMOVIC AINUNUE MWAKA 2003.
Claudio Ranieri-Septemba 2000 - Mei 2004
José Mourinho-Juni 2004 - September 2007
Avram Grant-September 2007 - Mei 2008
Luiz Felipe Scolari-Julai 2008 - Februari 2009
Guus Hiddink-Februari 2009 - Mei 2009
Carlo Ancelotti-Juni 2009 - Mei 2011
Andre Villas-Boas-Juni 2011 - Machi 2012
Roberto Di Matteo-Machi 2012 - ??

No comments:

Post a Comment