BUKOBA SPORTS

Tuesday, June 12, 2012

EURO 2012: ENGLAND V FRANCE " NGOMA SARE"

Ndani ya Uwanja wa Donbass Arena Mjini Donetsk Nchini Ukraine, England na France, zikicheza Mechi yao ya kwanza ya Kundi D la Fainali za EURO 2012, zilitoka sare ya bao 1-1.
England ndiyo waliotangulia kupata bao katika Dakika ya 30 baada ya frikiki ya Nahodha wao Steven Gerrard kuunganishwa kwa kichwa na Joleon Lescott.
Lakini, France, ambao katika Mechi nzima walimiliki mpira sana bila kuipasua ngome ya England, wakasawazisha kwa shuti la Samir Nasri akiwa nje ya boksi katika Dakika ya 39.

Baadae leo Timu nyingine za Kundi D, Sweden na Wenyeji Ukraine, zitakutana ndani ya Stadion NSK Olimpiyskiy Mjini Kiev Nchini Ukraine.
Mashabiki wa England wakishangilia baada ya kupata goli

Mechi zinazofuata za Kundi hili ni Ijumaa Juni 15 Ukraine itakapocheza na France na England kuivaa Sweden.Benchi la ufunsi la uingereza
Benchi la ufundi la Ufaransa chini ya kocha mkuu Laurent Blanc
VIKOSI
France: Lloris, Debuchy, Rami, Mexes, Evra, Nasri, Cabaye, Diarra, Malouda, Ribery, Benzema.
Akiba: Mandanda, Giroud, Matuidi, Reveillere, Menez, M'Vila, Martin, Ben Arfa, Valbuena, Clichy, Koscielny, Carrasso.
England: Hart, Johnson, Terry, Lescott, Cole, Milner, Gerrard, Parker, Oxlade-Chamberlain, Young, Welbeck.
Akiba: Green, Walcott, Henderson, Carroll, Baines, Jones, Jagielka, Downing, Defoe, Butland.
Referee: Nicola Rizzoli (Italy)

RATIBA:
Jumanne, Juni 12
KUNDI A
Wroclaw, Poland
Saa 1 Usiku
Greece v Czech Republic
Warsaw, Poland
Saa 3 Dak 45 Usiku
Poland v Russia
--------------------------
Jumatano, Juni 13
KUNDI B
Lviv, Ukraine
Saa 1 Usiku
Denmark v Portugal
Kharkiv, Ukraine
Saa 3 Dak 45 Usiku
Holland v Germany
------------------------
Alhamisi, Juni 14
KUNDI C
Poznan, Poland
Saa 1 Usiku
Italy v Croatia
Gdansk, Poland
Saa 3 Dak 45 Usiku
Spain v Republic of Ireland
----------------------
Ijumaa, Juni 15
KUNDI D
Kiev, Ukraine
Saa 1 Usiku
Ukraine v France
Donetsk, Ukraine
Saa 3 Dak 45 Usiku
Sweden v England
----------------------
Jumamosi, Juni 16
KUNDI A
Saa 3 Dak 45 Usiku
Wroclaw, Poland
Czech Republic v Poland
Warsaw, Poland
Greece v Russia
---------------------
Jumapili, Juni 17
KUNDI B
Saa 3 Dak 45 Usiku
Kharkiv, Ukraine
Portugal v Holland
Lviv, Ukraine
Denmark v Germany
---------------------
Jumatatu, Juni 18
KUNDI C
Saa 3 Dak 45 Usiku
Gdansk, Poland
Croatia v Spain
Poznan, Poland
Italy v Republic of Ireland
-------------------------
Jumanne, Juni 19
KUNDI D
Saa 3 Dak 45 Usiku
Donetsk, Ukraine
England v Ukraine
Kiev, Ukraine
Sweden v France

No comments:

Post a Comment