BUKOBA SPORTS

Tuesday, June 12, 2012

EURO 2012: ANDRIY SHEVCHENKO AWAMALIZA SWEDEN " MAMBO SAFI KWAO"

 Ni Mkongwe wa Miaka 35, Andriy Shevchenko, Jana usiku ameleta furaha kubwa Nchini kwao Ukraine ambao ni Wenyeji wenza wa EURO 2012 alipoinyanyua Ukraine toka bao 1-0 nyuma walipocheza na Sweden,
 ambao bao lao lilifungwa na Nahodha wao Zlatan Ibrahimovic, kwa kupachika bao 2 na kuwapa Ukraine ushindi wa bao 2-1 kwenye Mechi ya Kundi D la EURO 2012.
 
Sweden walitangulia kupata bao Dakika ya 52 lakini Dakika 3 baadae Shevchenko akasawazisha na Dakika 6 baadae akapiga bao la pili, yote yakiwa mabao ya kichwa.
 
Mechi inayofuata kwa Ukraine ni dhidi ya France na Sweden watacheza na England.
 SHABIKI LA SWEDEN
VIKOSI
Ukraine: 12-Andriy Pyatov; 9-Oleh Gusyev, 3-Evhen Khacheridi, 17-Taras Mykhalyk, 2-Evhen Selin; 4-Anatoly Tymoshchuk, 18-Serhiy Nazarenko, 11-Andriy Yarmolenko, 19-Evhen Konoplyanka; 7-Andriy Shevchenko, 10-Andriy Voronin
Sweden: 1-Andreas Isaksson; 2-Mikael Lustig, 3-Olof Mellberg, 4-Andreas Granqvist, 5-Martin Olsson; 6-Rasmus Elm, 9-Kim Kallstrom; 7-Sebastian Larsson, 10-Zlatan Ibrahimovic, 20-Ola Toivonen; 22-Markus Rosenberg
Referee: Cuneyt Cakir (Turkey)

No comments:

Post a Comment