BUKOBA SPORTS

Tuesday, June 12, 2012

REAL MADRID, MAN CITY, JUVENTUS KATIKA HARAKATI ZA KUMG'OA ROBIN VAN PERSIE ARSENAL!

Real Madrid imejiunga na Man City na Juventus katika Harakati za kuhakikisha mshambuliaji wa Arsenal, Robin Van Persie anang'oka katika klabu hiyo. Arsenal inajiandaa kumpa mkataba mpya van Persie, hata hivyo, awali walishindwana kimaslahi, lakini gazeti la "The Sunday Mirror" limeeleza kuwa, mshambuliaji huyo wa the Gunners hatasaini mkataba mpya timu hiyo na yupo tayari kununua sehemu ya mkataba wake wa mwaka mmoja uliobaki kuliko kuuzwa. Juve na Man City zinaongoza katika harakati hizo. Huku Real Madrid ikikaa mdomo wazi kumnyatia!

No comments:

Post a Comment