BUKOBA SPORTS

Monday, June 4, 2012

EURO 2012: GARY CAHILL NJE, KUTOKANA NA KUVUNJIKA TAYA SIKU YA JUMAMOSI NAFASI YAKE YACHUKULIWA NA MARTIN KELLY!


Gary Cahill hatacheza Fainali za EURO 2012 baada ya kuthibitika kuwa amevunjika Taya lake sehemu mbili.
Cahill aliumia Taya Siku ya Jumamosi England walipocheza Mechi ya kirafiki na Belgium baada ya Beki huyo kugongana na Kipa wake Joe Hart.


Gary Cahill hatacheza Fainali za EURO 2012 baada ya kuthibitika kuwa amevunjika Taya lake sehemu mbili.

Tayari England imeshamuita Beki wa Liverpool Martin Kelly ili kuchukua nafasi yake na sasa kinasubiriwa kibali cha UEFA kwa vile Siku ya mwisho kuwasilisha Majina ya Wachezaji 23 watakaocheza EURO 2012 ilikuwa ni Mei 29.

Kuumia kwa Cahill kunafanya idadi ya Wachezaji wa England walioumia na ikabidi waachwe kufikia wanne na wengine ni Kipa John Ruddy (alivunjika kidole), Viungo Gareth Barry (Musuli za tumboni) na Frank Lampard (Musuli za pajani).


ENGLAND =Timu iliwasilishwa UEFA hapo Mei 29:
Kocha: Roy Hodgson 
Makipa: Joe Hart (Manchester City FC), Robert Green (West Ham United FC), Jack Butland (Birmingham City FC).
Mabeki: Leighton Baines (Everton FC), Gary Cahill (Chelsea FC)==[KAONDOLEWA NAFASI KAPEWA Martin Kelly wa Liverpool], Ashley Cole (Chelsea FC), Glen Johnson (Liverpool FC), Phil Jones (Manchester United FC), Joleon Lescott (Manchester City FC), John Terry (Chelsea FC).
Viungo: Phil Jagielka (Everton FC), Stewart Downing (Liverpool FC), Steven Gerrard (Liverpool FC), Frank Lampard (Chelsea FC)==[KAONDOLEWA NAFASI KAPEWA Henderson wa Liverpool], James Milner (Manchester City FC), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal FC), Scott Parker (Tottenham Hotspur FC), Theo Walcott (Arsenal FC), Ashley Young (Manchester United FC).
Mafowadi: Andy Carroll (Liverpool FC), Jermain Defoe (Tottenham Hotspur FC), Wayne Rooney (Manchester United FC)*, Daniel Welbeck (Manchester United FC).
*ROONEY HACHEZI MECHI MBILI ZA KWANZA, AMEFUNGIWA

KUNDI D
Ukraine
Sweden
France
England
MECHI ZAKE = Kuchezwa Nchini Ukraine:
Juni 11: France v England [Mjini Donetsk Saa 1 Usiku]
Juni 11: Ukraine v Sweden [Kiev Saa 3 Dak 45 Usiku]
Juni 15: Sweden v England [Kiev Saa 1 Usiku]
Juni 15: Ukraine v France [Donetsk Saa 3 Dak 45 Usiku]
Juni 19: Sweden v France [Kiev Saa 3 Dak 45 Usiku]
Juni 19: England v Ukraine [Donetsk Saa 3 Dak 45 Usiku]

No comments:

Post a Comment