Dakika nne baadaye Mabingwa wa Dunia na Ulaya walifumania lango la Italia na licha ya juhudi na umahiri wa Mabeki David Silva alimuona Cesc Fabregas na kumuwekea pasi maridhawa na bila kufanya makosa akaupenyeza mpira kumpita goli wa Italia Buffon.
Kabla ya mashindano haya wadadisi walionelea kama Uhispania itakabiliwa na kibarua kigumu kutetea taji lake kutokana na wachezaji wake wengi kuwa wachofu mno. Jumla ya wachezaji 23 wa timu hii ya Taifa wamecheza jumla ya dakika 89,884 katika msimu uliopita ikilinganishwa na wenzao walioshiriki kwa upungufu wa dakika 17,000.
Timu mbili zilizomo kwenye kundi la C Jamhuri ya Ireland na Croatia lazima zimeridhishwa na matokeo haya zikiona kua na fursa ya kufanya vyema na uwezekano mkubwa wa kufuzu kutoka michuano ya makundi.
Mario Balotelli naye alikosa bao muhimu sana
Fernando Torres alikosakosa sana na alikuwa na nafasi nyingi za kufunga
Georgio Chielliniakipewa kadi ya njano
Pirlo na Xavi Hernandez wakichuana jana
Share: Eventually the spoils were split
VIKOSI
SPAIN: Casillas; Arbeloa, Ramos, Pique, Alba; Alonso, Busquets; Silva, Xavi, Iniesta; Fabregas
Akiba: Valdes, Albiol, Javi Martinez, Juanfran, Pedro, Torres, Negredo, Mata, Llorente, Santi Cazorla, Jesus Navas, Reina.
ITALY: Buffon; Bonucci, De Rossi, Chiellini; Maggio, Motta, Giaccherini, Pirlo, Marchisio; Cassano, Balotelli
Akiba: Sirigu, Ogbonna Obienza, Balzaretti, Abate, Di Natale, Barzagli, Borini, Montolivo, Giovinco, Diamanti, Nocerino, De Sanctis.
REFA: V Kassai (Hungary).
RATIBA MECHI ZINAZOFUATA:
Jumatatu, Juni 11
KUNDI D
Donetsk, Ukraine
[Saa 1 Usiku]
France v England
Kiev, Ukraine
Saa 3 Dak 45 Usiku
Ukraine v Sweden
No comments:
Post a Comment