Kwenye Difensi, kuna uwezekano mkubwa Masentahafu wakawa Joleon Lescott wa Manchester City na Nahodha wa Chelsea John Terry.
France itamkosa Kiungo Yann M'Vila ambae aliumia enka ingawa amepata nafuu na nafasi yake itachukuliwa na Alou Diarra au, ikibidi, Blaise Matuidi.
Akiizungumzia France, ambayo haijafungwa katika Mechi 21 na wameshinda jumla ya goli 9 katika Mechi zao 3 za mwisho za majaribio, Kocha wa England, Roy Hodgson, amesema:
“Lazima utambue kipaji chao wakishambulia. Ni hatari wakikaribia langoni kwako na kitu kikubwa ni kutafuta mbinu za kuzima hatari hiyo.”
Meneja wa France, Laurent Blanc, ameridhishwa na hali za Wachezaji wake na amewasifu Madaktari wake kwa kuhakikisha Wachezaji majeruhi, Yann M'Vila, Blaise Matuidi na Steve Mandanda, wamepona.
TATHMINI YA MECHI:
Jumatatu, Roy Hodgson akikaa Benchi la England, atakuwa ni Meneja wa kwanza Mwingereza kuiongoza England tangu Kevin Keegan afanye hivyo kwenye EURO 2000.
Kwa sasa France, nyota yao inang’ara mno na wanatinga kwenye EURO 2012 wakiwa hawajafungwa katika Mechi 21 huku wakiwa wameshinda Mechi 15.
Timu ya mwisho kuwafunga ilikuwa ni Belarus Mwezi Septemba, 2010.
Sifa zote hizo lazima apewe Meneja wao, Laurent Blanc, aliebatizwa jina la 'Le President' kwa uongozi wake wa uadilifu na thabiti.
Blanc, ambae aliichezea Manchester United, ameibadilisha Timu ya France kwa kuwachomeka Chipukizi Yohan Cabaye na Yann M'Vila, kutumia nguvu kazi ya Sentahafu Adil Rami, na utandazaji Soka na ufungaji wa Karim Benzema na Franck Ribery.
VIKOSI VINATARAJIWA:
ENGLAND: Hart, Johnson, Terry, Lescott, Cole, Milner, Gerrard, Parker, Downing, Welbeck, Young.
FRANCE: Lloris, Debuchy, Mexes, Rami, Evra, Cabaye, Diarra, Malouda, Nasri, Ribery, Benzema.
USO KWA USO
Mara ya mwisho kukutana kwenye Mashindano makubwa, France waliifunga England bao 2-1 kwenye EURO 2004 baada ya Frank Lampard kuipatia bao England na Zinedine Zidane kupachika bao 2 Dakika za majeruhi.
Kabla ya hapo walikutana kwenye EURO 1992 na kutoka sare 0-0.
Mara ya mwisho France kufungwa na England ilikuwa Tarehe 7 Juni Mwaka 1997 Alan Shearer alipopachika bao pekee.
RATIBA
Jumatatu, Juni 11
KUNDI D
Donetsk, Ukraine
[Saa 1 Usiku]
France v England
Kiev, Ukraine
Saa 3 Dak 45 Usiku
Ukraine v Sweden
----------------------
Jumanne, Juni 12
KUNDI A
Wroclaw, Poland
Saa 1 Usiku
Greece v Czech Republic
Warsaw, Poland
Saa 3 Dak 45 Usiku
Poland v Russia
No comments:
Post a Comment