BAADA ya kuiwezesha Chelsea kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa, mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich anafikiria kumpa kocha Roberto Di Matteo mkataba wa mwaka mmoja au zaidi kama majaribio.
Toka kuteuliwa kwa Roberto Di Matteo kuwa kocha wa muda wa Chelsea baada ya kufukuzwa kwa Andre Villas-Boas, kocha huyo wa zamani wa West Brom ameiongoza kutwaa Kombe la FA na lile la Mabingwa.
Lakini mafanikio hayo hayaonekani kumshawishi mmiliki wa timu hiyo kuwa Di Matteo anafaa kupewa kibarua cha kudumu kuifundisha Chelsea.
Hata hivyo Abramovich amekubali Di Matteo anastahili angalau mwaka mmoja zaidi wa kuifundisha Chelsea.
Uamuzi wa kumpa Di Matteo mwaka mmoja zaidi hautafikiwa hadi Mwanzoni mwa wiki hii. Hii inamaanisha kuwa Di Matteo ambaye amewahi kuichezea Chelsea ataenda mapumziko ya mwaka bila ya kujua mustakabali wake ndani ya Chelsea.
Inaaminika Di Matteo yuko tayari kuukubali mkataba huo wa mwaka mmoja au zaidi kama atapewa kwani hiyo itakuwa ni heshima kubwa sana kwake.
No comments:
Post a Comment