Timu ya Taifa ya Zanzibar leo huko Mjini Mjini Duhok, Iraq-Kurdistan itatinga Uwanja wa Duhok kucheza na Northern Cyprus katika Nusu Fainali ya KOMBE la DUNIA, rasmi kama VIVA 2012 World Cup, Mashindano ambayo ni mahsusi kwa wale ambao si Wanachama wa FIFA. Nusu Fainali nyingine ni kati ya Wenyeji Iraq-Kurdistan na Provence [France] ambayo pia itachezwa leo Ijumaa.
Fainali ni Jumamosi Juni 9.
Zanzibar ilitinga Nusu Fainali baada ya kushinda Mechi zake za Kundi B kwa kuzifunga Raetai [Swiss] bao 6-0 na Tamil-Eelam 3-0.
Kikosi cha leo cha Zanzibar kitakachoivaa Northern Cyprus ni:
Kipa: Abasi 2 Ismall Khamis 3 Otimani Tamim 4 Salum Said 5 Nadri Harub 6 Abdulhalim humud 7 Sulemani Kassim 8 Abdulghani Gulam 9 Abdi Kassim 10 Ali Badru 11 Khamis Mcha
MAKUNDI
KUNDI A:
- Kurdistan
- Occiatania [France]
- West Sahara
KUNDI B:
- Zanzibar
- Tamil-Eelam
- Raetia [Swiss]
KUNDI C:
- Northern Cyprus
- Provenza [France]
- Darfur
MATOKEO:
Juni 4
Kurdistan 6 Western Sahara 0
Zanzibar 6 Raetia [Swiss]
Northern Cyprus 15 Darfur 0
Juni 5
West Sahara 2 Occitania [France] 6
Raetia [Swiss] 1 Tamil Eelam 0
Darfur 0 Provence [France] 18
Juni 6
Occitania [France] 1 Iraq Kurdistan 2
Tamil Eelam 0 Zanzibar 3
Provence [France] 2 Northern Cyprus 1
No comments:
Post a Comment