BUKOBA SPORTS

Saturday, June 9, 2012

KOMBE la DUNIA 2012: ZANZIBAR 0 V 2 NORTHERN CYPRUS

Timu ya Taifa ya Zanzibar jana huko Mjini Mjini Duhok, Iraq-Kurdistan ilichapwa bao 2-0 na Northern Cyprus katika Nusu Fainali ya KOMBE la DUNIA, rasmi kama VIVA 2012 World Cup, Mashindano  ambayo ni mahsusi kwa wale ambao si Wanachama wa FIFA.
Nusu Fainali nyingine ilikuwa kati ya Wenyeji Iraq-Kurdistan na Provence [France] na  wenyeji hao kushinda bao 2-1.
Hivyo, leo Usiku, Zanzibar itacheza na Provence [Zanzibar] kusaka Mshindi wa 3 na Iraq Kurdistan itacheza na Northern Cyprus kwenye Fainali kumpata Bingwa wa Dunia.
Mechi zote mbili za leo zitachezwa Franso Hariri Stadium Mjini Arbil huko Iraq Kurdistan.
Zanzibar ilitinga Nusu Fainali baada ya kushinda Mechi zake za Kundi B kwa kuzifunga Raetai [Swiss] bao 6-0 na Tamil-Eelam 3-0.
Kikosi cha jana cha Zanzibar
Kipa: Abasi 2 Ismall Khamis 3 Otimani Tamim 4  Salum Said 5 Nadri Harub 6 Abdulhalim humud 7 Sulemani Kassim 8 Abdulghani Gulam 9 Abdi Kassim 10 Ali Badru 11 Khamis Mcha

MAKUNDI
KUNDI A:
- Kurdistan
- Occiatania [France]
- West Sahara
KUNDI B:
- Zanzibar
- Tamil-Eelam
- Raetia [Swiss]
KUNDI C:
- Northern Cyprus
- Provenza [France]
- Darfur
MATOKEO:
Juni 4
Kurdistan 6 Western Sahara 0
Zanzibar 6 Raetia [Swiss]
Northern Cyprus 15 Darfur 0
Juni 5
West Sahara 2 Occitania [France] 6
Raetia [Swiss] 1 Tamil Eelam 0
Darfur 0 Provence [France] 18
Juni 6
Occitania [France] 1 Iraq Kurdistan 2
Tamil Eelam 0 Zanzibar 3
Provence [France] 2 Northern Cyprus 1

No comments:

Post a Comment