BUKOBA SPORTS

Saturday, June 9, 2012

LEWANDOWSKI KUTUA MANCHESTER UNITED

Nyota wa Mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund, Robert Lewandowski, yupo mbioni kujiunga na Manchester United kufuatana na usemi wa Kocha wa Timu ya Taifa ya Poland Frank Smuda. 

Lewandowski, ambaye Msimu huu aliifungia Borussia Dortmund bao 30, Jana ameiongoza Nchi yake Poland kucheza Mechi ya ufunguzi ya EURO 2012 dhidi ya Greece.
Kocha Smuda amedai Nyota watatu wa Poland, Lukasz Piszczek, Kuba Blaszczykowski na Lewandowski, wote wako mbioni kuhama Klabu zao.

Amesema: "Kwa maoni yangu, watahama Borussia, 'Lewy' anakwenda Manchester United, Klabu fulani England, Piszczek anaenda Real Madrid. Wao wana malengo na wanataka kukua. Hapa Kikosi changu kinawategemea wao!"
Lewandowski bado ana Mkataba wa Miaka miwili na Dortmund lakini mazungumzo yake na Klabu hiyo ili kuboresha Mkataba wake yalivunjika hivi karibuni kwa madai Mchezaji huyo anataka kuhama. 

Tayari Man United ishamnasa Staa wa Japan Shinji Kagawa kutoka Dortmund na pia ipo mbioni kuwachukua Luka Modric wa Tottenham, Leighton Baines wa Everton na Kiungo wa Newcastle Cheick Tiote.

No comments:

Post a Comment