BUKOBA SPORTS

Monday, June 11, 2012

LEWIS HAMILTON AIBUKA MSHINDI MONTREAL JANA JUMAPILI!

Lewis Hamilton alifanikiwa kuwa mshindi katika mashindano ya Jumapili ya Grand Prix, akiandikisha rekodi ya mashindano msimu huu kushuhudia washindi mbalimbali wa msimu huu, akiwa ni mshindi wa saba, kwa ushindi huo wa Canada.
 
Muingereza Hamilton, ambaye ni dereva wa timu ya McLaren, alimtangulia Romain Grosjean, dereva wa Renault, na Sergio Perez, dereva wa Sauber, na aliyemaliza katika nafasi ya tatu.
 
Huku ikisalia mizunguko kumi kabla ya mashindano kumalizika, Hamilton alipambana kutoka nafasi ya tatu hadi ya kwanza, na akifanikiwa kumpita dereva wa Ferrari, Fernando Alonso, na pia wa Red Bull, Sebastian Vettel.
Madereva hao wawili waliamua kusimama mara moja kwa magari yao kukaguliwa, wakidhani mbinu hiyo itawasaidia, huku Hamilton akisimama mara mbili.
Leading from the front: Hamilton took back his lead late on after a second pit stop 
 Huu ni ushindi wa tatu wa Hamilton katika barabara za Gilles Villeneuve, na ushindi huo unamwezesha kuongoza kwa pointi katika kuwania ubingwa wa msimu huu wa mwaka 2012, akimshinda Alonso kwa pointi mbili, na Vettel, katika nafasi ya tatu, kwa pointi tatu.

And they're off: Sebastian Vettel led the charge from the front of the grid but slipped but to fifth by the end
 Sebastian

In a spin: Felipe Massa suffered an early setback when he spun off the track, only to recover

No comments:

Post a Comment