BUKOBA SPORTS

Monday, June 11, 2012

MCHEZAJI ALIETEKWA NIGERIA, CHRISTIAN OBODO - AOKOLEWA!

Klabu ya Udinese ya Italy imethibitisha kuwa Machezaji wao ambaye ni Kiungo wa Kimataifa wa Nigeria, Christian Obodo, ameokolewa na Polisi kutoka mikononi mwa Watekaji.
Obodo, Miaka 28, alitekwa nyara na Watu wenye silaha kwenye Mji wa nyumbani kwao Warri, Nigeria Jumamosi asubuhi wakati akiwa njiani kwenda Kanisani na Watekaji hao baadae waliitaka Familia yake ilipe Euro 150,000 ili aachiwe.

Taarifa ya Klabu ya Udinese imesema Polisi waligundua wapi Obodo amehifadhiwa na Watekaji hao kwa vile Simu yake ya mkononi ilikuwa wazi na ilielekeza wapi yupo.
Mara baada ya kuokolewa, Obodo alisema: “Namshukuru Mungu niko huru!”
Obodo, ambae alikuwa akiichezea Lecce kwa mkopo Msimu huu uliokwisha juzi, amekuwa akicheza Soka lake la kulipwa tangu kuanza Soka lake huko Italy na ameshawahi kuzichezea Timu za Perugia, Fiorentina na Torino.
Ameichezea Timu ya Taifa ya Nigeria mara 21.

No comments:

Post a Comment