Mahakama hiyo imesema itasikiliza maombi hayo Juni 25, mwaka huu, baada ya pande zote mbili kuwasilisha vielelezo kuhusiana nayo.
Umamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Dk. Fauz Twaib baada ya kutokea mabishano ya kisheria kati ya upande wa utetezi na Jamhuri kuhusu Mahakama kuchunguza umri halisi wa mshitakiwa kati ya miaka 18 iliyoandikwa kwenye hati ya mashitaka na miaka 17 kama inavyodaiwa na upande wa utetezi.
Jaji alisema kuwa, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, ilikosea kukataa kuchunguza umri wa mshitakiwa na kuamua kufutilia mbali amri iliyotolewa na Hakimu Augustina Mmbando.
Hakimu Mmbando alikataa kuchunguza umri wa Lulu na Mahakama Kuu imechukua jalada lake na itafanya yenyewe uchunguzi huo.
Alisema mawakili wa utetezi Florence Massawe na Peter Kibatala watawasilisha kwa njia ya maandishi vielelezo kesho na upande wa Jamhuri utajibu kwa njia hiyo ya maandishi Juni 20, mwaka huu na Mahakama kusikiliza Juni 25, 2012.
Katika kesi ya msingi, Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam, alimuua Kanumba.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), Lulu, hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Hata hivyo, baada ya upelelezi kukamilika, itahamishiwa katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Mapema jana saa 3:45 asubuhi, Lulu, alifikishwa katika viunga vya mahakama hiyo akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza.
Msanii huyo alikuwa amevaa suruari ya jeans rangi nyesi na blauzi nyeusi pamoja na kikoti maarufu kama kibajaji cha rangi ya zambarau huku akionekana kujiamini tofauti na awali alipokuwa akifikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment