BUKOBA SPORTS

Tuesday, June 5, 2012

MBUNGE WA BAHI OMARY BADWEL, AFIKISHWA KIZIMBANI LEO KWA KESI YA KUDAI RUSHWA


Mbunge wa Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel, akiwa chini ya ulinzi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili. Mbunge huyo alikamatwa jana kwa kile kilichodaiwa kudai na kutaka kupokea Rushwa baada ya kukamilika kwa mitego ya Wana TAKUKURU katika Hoteli ya Peacock iliyopo maeneo ya Mnazi Mmoja jana.
Mbunge wa Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel, akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wakati akitoka Mahakamani huku baada ya kusomewa mashitaka mawili ya rushwa ya sh. milioni 1, aliyokuwa akiitaka kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jonathan Liana.

Wakili wa Mbunge wa Bahi, Omary Ahmed Badwel, Mpare Mpoki (kushoto) akitoka Mahakamani.

Na Mwandishi Wetu, Jijini MBUNGE wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel (43) leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa kosa la rushwa ya shilingi Milioni moja toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jonathan Liana.

No comments:

Post a Comment