BUKOBA SPORTS

Monday, June 11, 2012

MWENYEKITI ARSENAL: SIWEZI KUHUHAKIKISHIA UMA KUMBAKISHA ROBIN VAN PERSIE!

ASEMA:- ‘Ni ngumu kupata Wachezaji waaminifu kama Giggs na Scholes!’

Mwenyekiti wa Klabu ya Arsenal, Peter Hill-Wood, amekiri hawezi kuhakikisha kuwa hawatamuuza Nahodha wao Robin van Persie ikiwa Fedha ndio zitakazoamua kubaki au kuondoka kwake.
Hill-Wood ametamka: “Yeye ni muhimu kwetu na amekuwa Nahodha mwema kwetu. Lakini akija Mtu na kumpa ofa Robin ya Mshahara wa Pauni 250,000 kwa Wiki nakiri hatuwezi kushindana na hilo!”

Aliongeza: “Kwa Wachezaji hujui nini watafanya. Wengine husema wanataka Mataji lakini wakipata nafasi ya kuchuma pesa zaidi, inabidi ubaki unaomba tu kuwa watabaki kwa sababu wana furaha walipo na waaminifu hapo walipo.”
Mwenyekiti huyo aliongeza zaidi kwa kusema: “Wachezaji kama Ryan Giggs na Paul Scholes huko Manchester United wamekuwa waaminifu kwa Klabu moja kwa kukaa maisha yao yote lakini hivi
sasa Wachezaji wa aina hiyo ni wachache mno!”
Hata hivyo Hill-Wood amesema bado wana matumaini watafikia makubaliano ya kurefusha Mkataba na Robin van Persie ambae Mkataba wake unamalizika baada ya Miezi 12.
Mwenyekiti huyo pia alisema baada ya kumsajali Lukas Podolski wana imani watasaini Wachezaji wengine wapya.
Hill-Wood alisema: “Naomba RVP abaki kwa Msimu ujao kwani nina hakika tutapigania Ubingwa wa Ligi Kuu. Msimu uliopita tulianza vibaya mno lakini tukabadilika na kumaliza nafasi ya 3 ambayo ni mafanikio mazuri hasa kwa vile tulikumbwa na maeruhi wengi.”
SOKA IN BONGO NEWS

No comments:

Post a Comment