Timu ya Taifa ya Uganda Cranes imejitahidi kuzima kitisho cha nyota wa Ligi kuu ya England waliomo kwenye Timu ya Teranga wa Senegal katika mchuano uliochezwa kwa kasi kwenye uwanja wa Mandela huko Nambole mjini Kampala.
Mabao ya Pappis Cisse na Godffrey Walusimbi yalitosha kuwalidhisha mashabiki wa Uganda Cranes nyumbani.
Bao la Senegal lilipatikana mnamo dakika 10 kabla ya kipenga cha mapumziko baada ya Ndoye Dane kuusuka mpira na kuwapita mabeki watatu wa Cranes upande wa kushoto na kutoa pasi kwa Papiss Demba Cisse aliyeuweka katika lango tupu kuipa Senegal matumaini.
Hadi mapumziko ni Senegal iliyohesabu bao 1-0 lakini Uganda Cranes ilirejea kipindi cha pili na nia ya kubadili mchezo.
Licha ya shinikizo kali zilizowaelekea wachezaji wa Simba wa Teranga Waganda walijitahidi hadi nusu saa baadaye ambapo Papa Sane alimuangusha Geoffrey Massa katika eneo la hatari na Refa kuonyesha alama ya tuta.
Hapa ndipo Godfrey Walusimbi alipojitokeza kuikoa Uganda Cranes na kumuelekeza kipa Sane upande mwingine na kuuchonga mpira upande wa pili.
Simba wa Teranga walicharuka lakini mashambulizi yao ya kushtukiza yalizimwa mnamo dakika za mwisho na mechi kumalizika kwa 1-1, hii ikiwa mechi ya pili katika kipindi cha wiki moja Uganda Cranes kumaliza mechi kwa sare ya 1-1 ambapo huko Angola walilazimisha matokeo kama hayo dhidi ya Angola.
No comments:
Post a Comment