Klabu ya Montpellier imethibitisha kuwa mazungumzo kuhusu uhamisho wa Mchezaji wao Olivier Giroud kwenda Arsenal yanakaribia kumalizika.
Dili ya kumchukua Straika huyo ambae yuko na Timu ya Taifa ya France huko Ukraine kwenye Fainali za EURO 2012 inatarajiwa kugharimu Pauni Milioni 10 na kila kitu kitakamilishwa akishamaliza michuano hiyo ya Ulaya.
Giroud, Miaka 25, Msimu uliopita alifunga bao 25 kwa Klabu yake Montpellier.
No comments:
Post a Comment