BUKOBA SPORTS

Tuesday, June 5, 2012

SHINJI KAGAWA ANYAKULIWA TAYARI NA MANCHESTER UNITED!

''YOSSO'' SHINJI KAGAWA
 
Klabu ya Manchester United imetangaza rasmi kumnasa Mchezaji wa Kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa, anaechezea  Borussia Dortmund ambao ndio Mabingwa wa Ujerumani.
 
Tangazo la kumnunua Kagawa, Miaka 23, limetoka muda mchache uliopita kwenye Tovuti ya Man United na limesema Klabu husika zishaafikiana kuhusu uhamisho wake na kilichobaki ni Mchezaji huyo kupimwa afya yake na kupatiwa Kibali cha Kazi cha Uingereza, taratibu ambazo zitakamilika mpaka ikifika mwishoni mwa Mwezi Juni.
 
Kagawa ndie anakuwa Mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Manchester United kwa ajili ya Msimu mpya wa 2012/13.
Msimu huu uliokwisha majuzi, Kagawa aliisaidia Borussia Dortmund kutwaa Ubingwa kwa kufunga mabao 13 kwenye Ligi ya Bundesliga na pia kuiwezesha kutwaa German Cup kwa kufunga mabao matatu.
Kwenye Fainali ya German Cup Borussia Dortmund iliifunga Bayern Munich 5-2 huku Meneja wa Man United Sir Alex Ferguson akiwa Uwanjani na Shinji Kagawa kubandika bao la utangulizi.


Shinji Kagawa
Birthdate: 17 March 1989
Position: Midfielder
Previous clubs: FC Miyagi Barcelona, Cerezo Osaka
Current club: Borussia Dortmund (transfer to United agreed, 5 June)

No comments:

Post a Comment