Haijapata kutokea Bingwa wa Mataifa ya Ulaya akafanikiwa kutetea vyema Taji lake na safari hii, huko Nchini Poland na Ukraine kuanzia Juni 8 hadi Julai 1 kwenye Fainali za EURO 2012, Mabingwa wa Ulaya Spain wana nafasi ya kufanya kile walichoshindwa Mabingwa 12 waliowatangulia-KUTETEA VYEMA TAJI LAO LA TAIFA BINGWA BARANI ULAYA!!
Spain wanatinga kwenye EURO 2012 wakiwa pia ni Mabingwa wa Dunia baada ya kutwaa Kombe la Dunia Mwaka 2010 huko Afrika Kusini na wapo Kundi C na Republic of Ireland, Croatia na Italy.
Spain wataanza kutetea Taji lao Juni 10 kwa kucheza na Italia.
Licha ya Bingwa mtetezi kuwa na kibarua kigumu cha kutetea Taji, kitu ambacho hakijawezekana, hata kufika Fainali huwa ni kazi ngumu mno na ni mara moja tu, Miaka 36 iliyopita, Bingwa Mtetezi alimudu kufika Fainali na kutandikwa kwenye Mechi hiyo na kuupoteza Ubingwa wake.
Hao walikuwa ni West Germany ambao walitwaa Ubingwa wa Ulaya Mwaka 1972 na kufungwa Fainali ya Mwaka 1976 na Czechoslovakia.
Bingwa mwingine mtetezi aliekaribia kutetea vyema Taji lake ni Soviet Union ambayo ilikuwa Bingwa Mwaka 1960, Mashindano ya kwanza kabisa ya Mataifa ya Ulaya, lakini kwenye Mashindano yaliyofuata, Mwaka 1964 huko Spain, Soviet Union walifungwa 2-1 na Spain.
HISTORIA YA UBINGWA WA ULAYA: | ||
MWAKA | MSHINDI | HATUA ALIYOFIKA MICHUANO ILIYOFUATA |
1960 | Soviet Union | MSHINDI WA PILI |
1964 | Spain | ROBO FAINALI |
1968 | Italy | ROBO FAINALI |
1972 | West Germany | MSHINDI WA PILI |
1976 | Czechoslovakia | MSHINDI WA TATU |
1980 | West Germany | MAKUNDI |
1984 | France | HAKUINGIA FAINALI |
1988 | Netherlands | NUSU FAINALI |
1992 | Denmark | MAKUNDI |
1996 | Germany | MAKUNDI |
2000 | France | ROBO FAINALI |
2004 | Greece | MAKUNDI |
2008 | Spain | ???????? |
No comments:
Post a Comment