
Na Mwandishi Wetu
MREMBO Brigita Alfred usiku wa kuamkia jana alitwaa taji la Redds Miss Sinza baada ya kuwashinda wenzake 13 katika kinyang’anyiro kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten Star Lounge).

Redd's Miss Sinza 2012, Brigita Alfred (katikati) akipunga mkono kwa furaha wakati akiwa na washindi wenzake, mshindi wa pili Judith Sangu (kushoto) na watatu Esther Mussa, baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza Jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Kampuni ya SPM-Sufiani Photo Magic na Mtandao wa Sufianimafoto.blogspot,com, Nasma Sufiani, akimvisha taji na kumkabidhi zawadi Maria John, baada ya kuibuka kidedea katika shindano la kumsaka Sufianimafoto Miss Talent, lililofanyika ndano ya shindano hilo la Miss Sinza katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza jijini Dar es Salaam.

Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya Tano Bora, wakipozi kwa picha, kutoka (kulia) ni Brigita Alfred, Judith Sangu, Nahma Said, Ester Mussa na Mariam Miraji, baada ya kutangazwa kutinga hatua hiyo. Brigita alionekana tokea mwanzo kuwa ataibuka uwa mshindi kwani aliuteka umati wa mashabiki wa masula ya urembo katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kinywaji cha Redds, Dodoma Wine, Lady Pepeta, Flexi P, Jackz Cosmetics, Clouds FM, sufianimafoto.blogspot.com na Screen Masters.
Kwa ushindi huo,Brigita alipewa shs 500,000 na tiketi ya kuiwakilisha Sinza katika mashindano ya Redds Miss Kinondoni. Mshndi wa pili katika kinyang’anyro hicho alikuwa Judith Sangu aliyezawadiwa sh. 400,000 na mshindi wa nafasi ya mshind wa tatu ilikwenda kwa Esther Mussa na kupewa shs. 300,000.
Mariam Miraji alishinda nafasi ya nne nay a tano ilikwenda kwa Nahma Saidi. Warembo wote hao watano walipata tiketi ya kushindana katika mashindano ya Miss Kinondoni.
Warembo wengine waliobaki, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Eva Mushi, Vailet John, Christina Samwel, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi na Merina Mushi walipewa zawadi ya kifuta jasho cha shs 100,000 ila mmoja katika shindano hilo lilopambwa na bendi ya African Stars wana Twanga Pepeta.
No comments:
Post a Comment