BUKOBA SPORTS

Saturday, July 14, 2012

KAGAME CUP: YANGA YAFUNGWA GOLI 2-0 NA TIMU YA ATLETICO


Mchezaji wa timu ya Yanga Juma Abdul akijaribu kunyang'anya mpira kutoka kwa beki wa timu ya Atletico Henry Mbazumutima kwenye mchezo wa pili wa fungua dimba katika michuano ya kombe la Kagame inayoandaliwa na shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki CECAFA inayofanyika jijini Dar es salaam Tanzania, Mpira umekiwasha na timu ya Yanga imeambulia kipigo cha magoli 2-0 yaliyofungwa na mchezji Didier Kavumbagu wa Atletico

Wachezaji wa timu za Yanga ya Tanzania na Atletico ya Burundi wakichuana vikali katika mchezo wao uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo.

Mashabiki wa mpira wakiwa kwenye uwanja wa Taifa kwa ajili ya kushuhudia pambano la michuano ya Kagame kwenye uwanja wa Taifa kati ya Yanga ya Tanzania na Atletico ya Burundi

Mashabiki wa timu ya Yanga wakiwa wamefurika uwanjani kwa ajili ya kushuhudia mchezo kati ya timu yao na timu ya Atleticokutoka Burundi.


MWANZA, MOROGORO KUCHEZA FAINALI COPA COCA-COLA 2012 KESHO
Fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inayozikutanisha timu za Mwanza na Morogoro itachezwa kesho (Julai 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanza saa 9 kamili alasiri.
Mwanza ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Temeke mabao 3-1 wakati Morogoro iliiondoa Tanga kwenye nusu fainali kwa ushindi wa mabao 3-1. Mechi zote za nusu fainali zilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Temeke na Tanga itachezwa kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 5 asubuhi. Mashindano ya Copa Coca-Cola 2012 yalianza Juni 24 mwaka huu yakishirikisha mikoa 28 ya Tanzania Bara na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment