BUKOBA SPORTS

Monday, July 23, 2012

EPIQ BONGO STAR SEARCH NDANI YA MBEYA - GREEN CITY - WAWAKUMBUKA WAHANGA YA AJALI YA BOTI ZANZIBAR KWA KUCHANGIA DAMU.


Mmoja ya washiriki akichangia damu kabla ya kuingia kwenye chumba cha sindano kwa majaji kuonyesha uwezo wake.
Usaili wa Epiq Bongo Star Search unaofanyika Club Vybes, Mbeya.Vitu muhimu vya kukumbuka ni majaji na washiriki wote walisimama kimya kwa dakika moja kuwakumbuka wahanga wa meli ya Mv. Skagit iliyozama Zanzibar. Vijana wengi wamejitokeza kwenye usaili. Shighuli ya uchangiaji damu pia unafanyika Club Vybes na washirki wameonyesha muamko mzuri kwenye shughuli hii. Usaili utafanyika leo na kesho Club Vybes, Mbeya na mwisho wa siku ya kesho tutakuwa tumewapata wawakilishi wa Mbeya.


Majaji wa Epiq BSS - Madam Ritha, Salama na Master Jay wakisimama kwa dakika 1 kuwakumbuka wahanga wa ajali ya boti iliyotokea Zanzibar.

Umati wa vijana wenye vipaji wakitafuta nafasi ya kufunguka na Epiq Bongo Star Search


Baadae waliendeleza zoezi la kufuatilia vipaji ambapo pia walitoa elimu kwa washiriki waliojitokeza katika usaili mkoani hapo.
Foleni ya Vipaji vya BSS ikijiandaa kusailiwa ndani ya uwanja wa CCM Kirumba
Umati uliojitokeza ukisubiri kusailiwa ndani ya uwanja wa CCM Kirumba
Hili ni eneo la kujiandikisha



Vijana mbalimbali waliojitokeza leo wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kuingia chumba cha usaili kwenye uwanja CCM Kirumba jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment